ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, September 13, 2015

WATOTO WENYE MARADHI YA SARATANI WANUFAIKA NA LISHE BORA

Meneja Mawasiliano na Matukio wa Vodacom Tanzania, Christina Chacha(wapili toka kushoto) akifurahia jambo na mtoto Anna Rajabu anayelelewa na kupata matibabu ya Saratani katika kituo cha Tumaini la Maisha katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Wakati wafanyakazi wa Vodacom Tanzania walipowatembelea na kuzindua mradi wa lishe bora kwa watoto hao wenye kusumbuliwa na maradhi hayo. Ambapo Taasisi ya Vodacom Foundation imetoa msaada wa kiasi cha shilingi milioni 26 kwa ajili ya kusaidia watoto hao kupata huduma za lishe bora katika kituo hicho.kulia ni mama mzazi wa mtoto huyo Bi.Mwanaidi Rajabu.
Mtoto Jovin John(2) ambaye ni mgonjwa wa saratani akishirikiana na Ofisa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Glory Mtui kujenga wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa saratani na kuzindua mradi wa lishe bora kwa watoto hao wanaotibiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Ambapo Taasisi ya Vodacom Foundation imetoa msaada wa kiasi cha shilingi milioni 26 kwa ajili ya kusaidia watoto hao kupata huduma za lishe bora katika kituo hicho.
Ofisa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Glory Mtui ( wapili kutoka kushoto)pamoja na Mama mzazi wa Jovin John(2) wakimshuhudia mtoto huyo akijenga anayepata matibabu ya ugonjwa wa saratani katika Kituo cha Tumani la Maisha kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa huo na kuzindua mradi wa lishe bora kwa watoto hao wanaotibiwa katika hospitali hiyo. Ambapo Taasisi ya Vodacom Foundation imetoa msaada wa kiasi cha shilingi milioni 26 kwa ajili ya kusaidia watoto hao kupata huduma za lishe bora katika kituo hicho.
Amos Joachim ambaye ni mmoja wa watoto wanaotibiwa ugonjwa wa saratani katika kituo cha Matumaini ya Maisha kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam (kulia) akicheza na mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Klemie Majamba (kushoto)wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea watoto hao wanaosumbuliwa na ugonjwa huo na kuzindua mradi wa lishe bora kwa watoto hao wanaotibiwa katika hospitali hiyo. Ambapo Taasisi ya Vodacom Foundation imetoa msaada wa kiasi cha shilingi milioni 26 kwa ajili ya kusaidia watoto hao kupata huduma za lishe bora katika kituo hicho.
Mkuu wa Taasisi ya Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza akishirikiana kucheza michezo mbalimbali na watoto wanaopatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani katika Kituo cha Tumani la Maisha kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa huo na kuzindua mradi wa lishe bora kwa watoto hao wanaotibiwa katika hospitali hiyo. Ambapo Taasisi ya Vodacom Foundation imetoa msaada wa kiasi cha shilingi milioni 26 kwa ajili ya kusaidia watoto hao kupata huduma za lishe bora katika kituo hicho.

Watoto wanaosumbuliwa na maradhi ya saratani ambao wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamepatiwa msaada wa lishe ili kupunguza tatizo la kupata lishe duni ambalo limekuwa tatizo sugu linalowaathiri watoto wengi nchini.

Ukosefu wa chakula bora chenye virutubishi vinavyotakiwa mwilini ni moja ya tatizo ambalo limekuwa likipelekea watoto wengi kunyemelewa na magonjwa mbalimbali kutokana na kupunguza kinga ya mwili na wale wenye magonjwa kuchelewa kupona kutokana na lishe duni.

Msaada huo wa lishe umetolewa mwishoni mwa wiki katika wodi ya watoto ya hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kuwahudumia watoto wenye maradhi ya Saratani linalojulikana kama Tumaini la Maisha.

Akiongea wakati wa kupokea msaada huo Mratibu wa mradi huo Dk.Jane Kaijage alishukuru msaada huo kutoka Vodacom Foundation kwa watoto utakaowafikia na kuwanufaisha walengwa kupitia taasisi ya Tumaini la Maisha.

Alisema kuna idadi kubwa ya watoto zaidi ya 300 wanaolazwa hospitalini hapo wakiwa wanakabiliwa na saratani ya aina mbalimbali na kutokana na umri wao lishe bora ni muhimu kwao sambamba na matibabu wanayoendelea kuyapata ili wapone haraka.

Kwa upande wake Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza alisema kuwa siku zote taasisi hiyo itakuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali katika kusaidia jamii hususani katika nyanja za Afya na Elimu.

“Afya ni moja ya suala ambalo tunalipa kipaumbele na ndio maana tumekuwa tukivalia njuga kutokomeza magonjwa mbalimbali mojawapo ikiwa ugonjwa huu wa saratani ambao siku hadi siku umekuwa ukiongezeka na kusababisha vifo vya watu wengi”Alisema.

Alisema Vodacom Foundation imetoa kiasi cha shilingi milioni 26 kupitia taasisi ya Tumaini la Maisha ili kuwawezesha watoto hawa kupatiwa chakula bora na matunda kwa ajili ya kuwajengea afya bora hususani katika kipindi hiki kigumu wanachoendelea kupata matibabu na aliwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia wenye matatizo mbalimbali kwenye jamii.

Mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake anaendelea na matibabu ya Saratani Jane Paulo kutoka mkoani Kigoma akiongea kwa niaba ya wenzake alishukuru Vodacom Fondation kwa msaada huu muhimu wa lishe kwa watoto wao katika kipindi hiki kigumu ambacho wanaendelea kupata matibabu.

Alisema kwa msaada huo taasisi hiyo imethibitisha usemi wa akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki kwa kuwa umetolewa katuka muda mwafaka ambao watoto wanahitaji kupata lishe bora wakati huo wazazi wengi wakiwa wanakabiliwa na changamoto ya kutomudu kununua vyakula muhimu kutokana na kukabiliwa na ugumu wa maisha ambao unasababishwa na kutumia muda wao mwingi kuuguza watoto badala ya kujishughulisha na kazi za kuwaingizia vipato.

1 comment:

Anonymous said...

Pesa za safari moja tu ya JK ya kusafiri nje ya nchi ingeweza kuwasaidia watoto hawa kwa miezi sita!!
Poleni sana wadogo zetu mabadiliko yanakuja!.