Askofu wa kanisa Katoliki,
siku ya trh 26-09-2015 alinukuliwa akitaja sifa za mgombea anaepaswa kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano Tanzania.
1. Mwadilifu
amesema nchi yetu ilipofika inahitaji mtu/rais ambaye anao uadilifu wa kweli na wa hali ya juu ili kuleta uongozi uliojaa uadilifu na nidhamu katika kuhakikisha kuwa watanzania wananufaika na kufurahia nchi yao na mambo yake yote.
2. Uchapa kazi kwa vitendo na Nidhamu,
nchi hii inayo rasilimali za kutosha ambapo zikitumika vyema watanzania watanufaika na maisha yao yatakuwa pazuri sana zaidi ya sasa hivi. Ili kuhakikisha hayo ni lazima tupate kiongozi mchapa kazikwa vitendo na hata tukimuuliza umefanya nini anao uwezo wa kutuambia nimefanya hili na lile.
3. Mtekeleza majukumu yake ipasavyo
kiongozi ambaye atakua Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania anapaswa kuwa ni mtekeleza majukumu anayopewa na yanayomhusu ipasanyo, kama umekabidhiwa jambo unalifanya kwa ukamilifu wake. Hivyo tanzania ya sasa haihitaji tena wajanjajanja ambao wanachekea watu huku hakuna utekelezaji wa majukumu yao ipasavyo.
4. Mzalendo
hakuna maendeleo tuyatakayo hapa nchini kwasababu viongozi wetu wengi sio wazalendo wa kweli, wanayoyasema hawayaishi, wanayoyahidi hawayatekelezi kisawasawa.
Hivyo basi 2015-2020 inahitaji wazalendo wa kweli na naamini mpaka sasa tumeona nani mzalendo anayezungumza kwa ukali na umakini kuwa atawasaidia watanzania na atapambana na ufusadi, wezi na kushughulika na wabadhilifu wa mali na uchumu wa nchi.
5.Mcha Mungu
katika utumishi uliotukuka na katika utumishi uliojaa haki na utawala makini na bora ni lazima tupate rais ambaye anayo hofu ya Mungu na nimcha Mungu kabisa. Mwaka huu watu wanaoigiza kuwa niwacha Mungu wanapaswa kukataliwa kabisa.Tuwachague watu wanaoonekana kuwa na hofu ya Mungu.
6.Mpenda watu
kupendwa na watu pia ni sifa muhimu sana, ila uwe unapendwa sio kwasababu unawapa rushwa, sio kwasababu uliwaandaa muda mrefu wakupende, sio wakupende kwasababu umewafanya watamani kumkomesha mtu au chama fulani. Iwe wanakupenda kwasababu ni mtendaji wa kazi, kwasababu unachukiwa wezi mafisadi, uwe wanakupenda kwasababu hupendi mchezo ktk kazi, iwe wanakupenda kwasababu ya uzalendo wako. Nawe pia uwe unawapenda kwasababu unayapenda maelendeleo yao na uwe unawapenda kwa kuwatendea kazi ipasavyo na sio kuwaibia mali zao.
7. Asiwe boss kwa wananchi
rais ajaye hapaswi kuwa boss/ meneja wa wananchi wake. Hii ni tabia chafu kwa rais kuwa au kujifanya boss au meneja wa taifa zima. Bali rais anapaswa awe mtumishi wa watu, achukue muda wake mwingi kuwazungukia wananchi katika maeneo yao kukagua shughuli za maendeleo na kushiriki pia, hivyo lazima uwe mkakamavu wa mwili na akili.
8.Ujasiri wa kuwakemea wasio waadilifu
rais wa tanzania 2015-2020 anapaswa kwa nguvu zote awe mjsiri wa kukemea na kuwaonya hata kuwachukulia hatua viongozi na watanzania wasio waadilifu. Ni lazma afanye hivyo kwa lengo la kujenga nchi yetu katika hali ya uadilifu ili kuimarisha umoja,mshikamano, ushirikiano hata usawa na haki. Tayari mmeshaona kiongozi mwenye ujasiri wa kufanya hivyo, na hata anayekerwa na wasio waadilifu.
Kwa kuzingatia hayo tutakuwa tumepata kiongozi chaguo la Mungu 2015-2020
5 comments:
Those in the glass house should never through rocks. He was implicated in the escrow scandal, he should stay quite. Bishop/ Cardinal should not be involved with corruption
Nonsense!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
You should never opt to express yourself in English, because you lack the requisite fluency of the language!
CCM Oyeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!
CCM juu zaidi!!!!!!!!
Post a Comment