Monday, October 26, 2015

MATOKEO YA AWALI MAGUFULI AONGOZA KWA SILIMIA 65 DHIDI YA LOWASSA


4 comments:

Anonymous said...

Vijimambo nipelekeeni salaam zangu kwa wacheza kamari wasiotumia akili - Kingunge, Sumaye, Mwapachu, Msindai, Mgeja na wengine. Wapeni pole nyingi sana kwa sababu imekula kwao. Inaonekana hata fifth graders are more politically astute than these career politicians. What a bummer? Njaa na tamaa ni vitu vibaya sana!

Unknown said...

Imani yetu kwamba bila ya kufuata ushabiki watanzania wangemchagua mgombea stahiki kwa mahitaji ya matatizo yao sio mahitaji ya mgombea na kwa kiasi fulani dalili zinaonesha watanzania hawaja tuangusha.

Anonymous said...

Hali hii kweli inaonyesha jinsi Watanzania wengi ni makini na hawayumbishwi na siasa uchwara ambazo viongozi wengine walikuwa wanatumia ili kuwaghiribu akili kwa manufaa yao binafsi. Kwa kutumia akili zao za kuzaliwa wamewadhihirishia wale wanaojidai kuwa wamesoma sana kwamba pamoja na elimu yao ya kidunia wao wanaona mbali zaidi hivyo kwao haikuwa lazima wawe na kisomo cha juu sana kama ambavyo wao wamekuwa wanajivunia. Nawapa hongera zangu nyingi sana Watanzania wenzangu kwa hili na wala tusikubali hata siku moja kuyumbishwa na watu ambao hawana mpango na maslahi ya nchi yetu zaidi ya maslahi yao tu. Pamoja na kuwa matokeo yote hayajatoka naamini hata hivyo kuwa mambo mpaka sasa yanaelekea upande wetu tulio wengi kwani Waswahili walisema, "dalili za mawingu ni Mua" na hivyo tutarajie tu kuwa hivi karibuni tuta sherehekea ushindi.

Anonymous said...

Kimbunga cha Lowassa na Chadema na wengineo kitaanza kuishiwa nguvu ya upepo; takataka zote zitaanza kuanguka chini moja moja! Uchambuzi yakinifu na wa ndani tutaufanya baada ya kutangaza mshindi.