Stanslaus Mabula akiongea na wanahabari baada ya kutangazwa mshindi wa Ubunge Jimbo la Nyamagana (CCM)
Na George Binagi-GB Pazzo
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la
Nyamagana Mkoani Mwanza ameibuka mshindi wa kiti cha Ubunge katika jimbo hilo
kwa kupata kura 81,017 na hivyo kumbwaga aliekuwa mbunge wa jimbo hilo Ezekiel
Wenje kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema aliepata kura 79,280.
Matokeo hayo yalitangazwa na Msimamizi Mkuu wa
Uchaguzi Jimboni humo ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Tito
Mahinya huku kukiwa na Ulinzi Mkali wa vyombo vya ulinzi na usalama katika
viunga vya ofisi za Jiji hilo.
Kwa upande wa Wagombea wengine, Chacha Okong’o
(ACT Wazalendo) alipata kura 161, Faida Potea (CUF) amepata kura 1,005, Ahmad
Mkangwa (NRA) kura 104, Mohamed Msanya (Jahazi Asilia) kura 175 na Ramadhan
Mtoro (UDP) amepata kura 68.
Hata hivyo kabla ya matokeo hayo kutangzwa, Mgombea
kutoka Chadema Ezekiel Wenje alikataa kusaini karatasi ya wagombea na kubainisha
kuwa demokrasia haikutumika katika zoezi zima la uhesabuji wa kura katika
uchaguzi huo na kwamba atafuata hatua zaidi za kisheria katika kupinga matokeo hayo.
Kwa upande wake Mshindi wa Uchaguzi huo
Stanslaus Mabula alisema kuwa tangu awali alitarajia ushindi huo na kwamba suala
la demokrasia limezingatiwa.
Katika hatua nyingine Mabula alibainisha kuwa
atahakikisha anatatua changamoto zinazolikabiri Jiji la Mwanza ikiwa ni pamoja
na kuwaunganisha wakazi wa Jiji katika shughuli mbalimbali za uzalishaji ili
waweze kujitegemea kiuchumi.
Ezekiel Wenje akiongea na wanahabari muda mfupi kabla ya matokeo kutangazwa
Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jijini Mwanza Titho Mahinya akitangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu Jijini Mwanza
Kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana akiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (kulia) muda mfupi kabla ya matokeo kutangazwa
1 comment:
CCM juuu kwa juuu.
Post a Comment