balozi_CLIPCHAMP_keep from Luke Joe on Vimeo.
Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Uwakilishi wake wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, umekemea mwenendo na tabia zinazofanywa na baadhi ya Asasi zisizo za kiserikali za kupotosha ukweli kuhusu changamoto zinazowakabili watu wenye ualibino lakini kubwa zaidi kutaka kujinufaisha kupitia matatizo yao.
Aidha Tanzania, pamoja na kukiri kwamba kuna tatizo la watu wenye ualibino la kupoteza maisha au kukatwa viungo imetoa ufafanuzi wa kile kinachoonekana kuelezwa na baadhi ya asasi hizo kwamba, ama serikali haijafanya jambo lolote kukabiliana na changamoto hiyo na au, watanzania na serikali yao wamelifumbia macho kiasi ambacho sasa kuhitaji msukumo zaidi kutoka mataifa ya nje.
Maelezo na ufafanuzi huo umetolewa siku ya jumatano na Balozi Tuvako Manongi, wakati akizungumza na wawakilishi wa muungano wa waandishi wa habari wanaofanya kazi zao hapa Umoja wa Mataifa.
Ufafanuzi na maelezo hayo umetolewa kufuatia taarifa zilizoufikia Uwakilishi wa Kudumu za kuonyeshwa kwa filamu inayoelezea changamoto zinazowakabili watoto wenye ualibino.
Filamu hiyo ijulikanayo kama A Boy from Geita, itaonyeshwa alhamisi jioni na fursa ya kuonyeshwa katika Umoja wa Mataifa imefadhiliwa na Uwakilishi wa Kuduma wa Canada kwa ubia na baadhi ya Idara za Umoja wa Mataifa pasi kuujilisha au kuhusisha Uwakilishi wa Tanzania ili hali filamu hiyo inahusu Tanzania.
Kwa mujibu wa Muandaaji wa filamu hiyo, maelezo yanayotolewa kama maudhui ya filamu siyo tu kwamba ni ya upande mmoja kwa maana ya kuwa Serikali au mamlaka husika haikupewa fursa ya kuelezea juhudi zake. Inaeleza kwamba watoto wenye ualibino wanaishi katika hofu kubwa katika kila siku ya maisha yao.
Kama hiyo haitoshi, muandaaji wa filamu hiyo inayomhusisha pia raia mmoja wa Canada Bw. Peter Ash kama mhusika mkuu pamoja na mtoto huyo wa Geita Adam anasema, aliamua kusafiri kwenda Afrika (Tanzania) kujielimisha zaidi kuhusu vitendo hivyo vya kikatili na alichojifunza ni kuwa watoto wenye ualibino wanauzwa kwa watu wanaotafua viungo vyao na mara nyingi huuzwa na wazazi wao.
“ Filamu hii inalenga kutoa mwanga wa hali halisi wanayokumbana nayo kila siku watu wenye ualibino nchini Tanzania . Inalenga kuleta mabadiliko na kutokemeza janga hilo, utashi wa kisiasa na msukumo kutoka mataifa ya nje ni wa lazima” kwa mujibu wa muaandaji wa filamu.
Kama hiyo haitoshi, muaandaji anataka kuuelezea ulimwengu kwamba ujinga ni laana inayowasumbua waaafrika na hivyo kuwaelimisha ndiyo jibu sahihi na kwamba filamu hiyo ni kusherehekea kazi nzuri ya wacanada ambao kupitia uwezo wao wanaweza kuleta mabadiliko.
Balozi Manongi amewaambia waandishi hao kwamba, maelezo na maudhui mazima ya filamu hiyo siyo tu yanalenga katika kupotosha na kupindisha ukweli, lakini pia kutotoa nafasi kwa serikali kuelezea juhudi inazofanya jambo ambalo si sawa.
Akasema , serikali ya Tanzania kuanzia kiongozi wake wa juu, Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kushirikiana na vyombo vyake vya sheria, vyama vya watu wenye ualibino, wadau mbalimbali na wananchi imejitahidi sana katika kukabiliana na tatizo hilo.
Akasema serikali inakaribisha ushirikiano wa wadau mbalimbali, na kwamba tatizo linalowakumba watanzania wanaoishi na ualibino haliwezi kumalizwa kwa kuonyesha filamu na kubwa zaidi kupindisha ukweli kwa manufaa ambayo kwa kiasi kikubwa yanakwenda kwa waandaaji wa filamu hizo kuliko walengwa.
Katika kuonyesha ni kwa kiasi gani serikali inaendelea na jitihada zake za kukabiliana na tatizo linalowakumba watu wenye ualubino. Balozi alitoa takwimu zinazoonyesha namna gani serikali inavyoguswa na kuchukua hatua.
“Hatukanushi kwamba hakuna matendo ya kikatili dhidi ya watanzania wenzetu wenye ualibino. Kuanzia mwaka 2006 mpaka sasa jumla ya watu 139 wanaotuhumiwa kujihusisha na ukatili huo walikamatwa, 35 kati yao walifikishwa mahakamani, kesi 25 zimekamilika, 15 wamehukumiwa na 75 waliachiwa baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha ili hali 13 kati ya waliohukumiwa wamepewa adhabu ya juu kabisa ambayo ni kunyongwa” akasisitiza Balozi
Vile vile Balozi amesema Tanzania pia imeridhia sheria mbalimbali za kimataifa, zikiwano za haki za binadamu na kwamba kwa kushirikiana na Chama cha watu wenye ualibino (TAS) huadhimisha kila mwaka siku ya watu wenye ualibino tangu mwaka ambayo 2006.
2 comments:
CCM ndo wanunuzi wakubwa WA viuongo vya albino
Kisa wao wako serikalini na zunasusua tu
Lowassa Lowassa mgonjwa mwenzetu tukombowe
Wacha maneno yasiokuwa na busara. Kama huna hoja kaa kimya.
Post a Comment