Kamanda wa
Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP),Suleiman Kova akionyesha silaha kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani)walizozikamata kutoka kwa majambazi katika operesheni ya jeshi hilo
iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Na Chalila
Kibuda
JESHI la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limevunja kambi inayodaiwa kuendesha
uhalifu wa kigaidi wa kuvamia vituo vya polisi na kunyanganya silaha kwa ajili
ya kuendeleza uhalifu na kuweza kukamata watuhumiwa saba.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum
ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP),Suleiman Kova amesema kundi
limenaswa kutokana na taarifa mbalimbali k mauaji ya kinyama na uporaji
silaha.
Amesema
kundi hilo linalodaiwa kuendeshwa na familia moja ya Ulatule limekuwa
likiendesha matukio mengi ya uhalifu ya kupora silaha katika vituo
vya polisi.
Majambazi
hao walikamatwa wakiwa na bunduki nne pamoja na risasi 18 aliwataja
majina watuhumiwa hao kuwa ni Saidi Mohamed Ulatule (67) ‘Uso a wa Simba’ ,
Mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga mkoa wa Pwani,Ramadhan Ngande (29)Miaka 29,
Dereva wa Bodaboda, Mkazi wa Kongowe,Hamis Ulatule (51),Mkulima, Mkazi wa
Mamdimkongo, Mkuranga, Pwani,Alli Ulatule(65), Mkazi wa Mamdimkongo, MKuranga,
Pwani,Nassoro Ulatule (40), Mkazi wa Mamdimkongo, Mkuranga, Pwani,Seleman
Ulatule (83),Mkazi wa Mamdimkongo, Said Chambeta (40) ‘Mzee wa
Fasta’Mfanyabiashara wa Mitumba, Mkazi wa Yombo Makangarawe kati yao Mtuhumiwa
wanne ni wa familia moja inayojihusisha na vitendo vya ujambazi pamoja na
vya kigaidi.
Wakati huo
Jeshi la Kanda Maalum ya Dar es Salaam,limewakamata watuhumiwa sita wa mauaji
wa Askari wa kikosi cha kupambana na uhalifu Morogoro,Elibariki Pallangyo
lilolofanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar es Salaam.
Kova amesema
katika tukio la kukamata watu hao kiongozi wao, Omary Salehe (Bonge Mzito)
alisema kuna silaha ikiwa ni njia ya kutaka kutoroka katika mikono ya polisi
ambapo polisi walitumia mafunzo yao vizuri na kufanikisha kumjeruhi na
alifariki wakati akipelekwa Hospitali.
Wengine ni
Said Mazinge (37) Mkazi wa Tegeta Kibaoni
Rashid
Watson (21)‘Dodo’Mkazi wa Vingunguti, Ramadhan Salum (38)’Nguzo
Mkazi wa Mbagala Kiburugwa Bakari Rashidi (38) ‘Malenda’
Mkazi wa Mbagala kizuiani Hamis Hamis (24) ‘Freemason Mkazi wa
Mbezi .
CHANZO: MICHUZI BLOG
No comments:
Post a Comment