Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya |
Jeshi la Polisi Mkoani
Mbeya limetoa rai kwa wafuasi wa vyama vishiriki katika uchaguzi mkuu Octoba 25
mwaka huu kujiepusha kufika katika
kituo cha kupigia kura wakiwa wamevaa nguo zenye picha za wagombea, maneno au
nembo ama rangi za chama cha siasa.
Aidha wametakiwa , kuepuka
kutumia uvumi, maneno ya uongo, hisia au visingizio vyenye lengo la kuwazuia
wengine kwenda kupiga kura.
Pia amewataka kuepuka
kufanya kampeni katika kituo cha kupigia kura iwe kwa maneno ya ushawishi au
kwa kuonyesha ishara ya chama fulani cha siasa.
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ahmed Msangi
amesema nivema kila mwananchi anae stahili kupiga kura ahakikishe anafuata
taratibu hizo ili kujiepusha na vitendo vya uvujifu wa amani katika siku hiyo
muhimu.
Amesema vyema kila mwananchi kupiga kura kwa kutumia
jina na kitambulisho chake na sio cha mtu mwingine, aliyekufa au mgonjwa, kuepuka
kufanya fujo ama vurugu katika kituo cha kupigia kura.
Aidha amesisitiza kuwa kila
mpiga kura mara baada ya kupiga kura kuondoka kwenye kituo cha kupigia kura na
kuendelea na shughuli nyingine kwani ni kosa kupiga kura na kuendelea kubaki
katika eneo la kituo cha kupigia kura.
Amesema ni wajibu wa jeshi la polisi kuwalinda maofisa
wanaosimamia uchaguzi, kuhakikisha kwamba zoezi la upigaji kura linaenda sawa,
bila vikwazo au bughudha na kuhakikisha vifaa vya kupigia kura viko salama.
Kwa mkoa wa mbeya tuna
jumla ya majimbo 13 ya uchaguzi, vituo 3,899 vya kupigia kura, kila kituo
kitalindwa na askari ili kuhakikisha suala la ulinzi na usalama linaimarishwa
kwa kipindi chote cha zoezi la kupiga kura, kuhesabu kura na kutangaza matokeo
ya uchaguzi.
Msangi amesema Jeshi la
polisi mkoa wa mbeya limejipanga kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ikiwa ni
pamoja na vituo vya kupigia kura sanjali na kuwepo kwa na doria za magari, pikipiki, mbwa na askari
ambao watakuwa wakitembea huku na kule kwa lengo la kudhibiti vitendo vyovyote
vya uvunjifu wa amani.JAMIIMOJA BLOG
4 comments:
ASANTE.KAMANDA MSANGI UNAJIREKEBISHA SASA,AU UMEONA MOTO UMEKUWAKIA VIBAYA?MAELEZO YAKO KAMANDA NI MAZURI TUNAYAUNGA MKONO,NDANI YAKE HAKUNA HILA WALA VITISHO,UNAWAHIMIZA RAIA WALIOJIANDIKISHA KUPIGA KURA WAFANYE HIVYO,KWA UJUMLA NI TAARIFA YA KIISTAARABU.UOVU MKUBWA KUPINDUKIA UPO DAR-ES-SALAAM[MKUU WA MKOA],DODOMA [RPC NA MKUU WA MKOA],MWANZA[RPC NA MKUU WA MKOA], NA SINGIDA[RPC NA MKUU WA MKOA].TUPO MAKINI TUKISUBIRIA MWISHO WA SIKU.CCM WANAOGELEA KUTAKA KUYAPISHA MAWIMBI-ANGAMIZI.SIMULIZI ZINAKUJA.
KAMA KAWAIDA..UKAWA MNAONEWA DODOMA, MWANZA, DAR, ETC! NAONA MAFURIKO YA MVUA YANAWAPATA AND YOU ARE TRYING TO EXPLOIT ALL POSSIBLE EXCUSES FOR YOUR LOSS TOMORROW OCT.25? CRY BABIES MENTALITY, POOR UKAWA/CHADEMA!
WEWE KWELI NI BASTARD,UKO HUMU NCHINI KWELI WAKATI UNAPOFYATUKA NA UTUMBO WAKO HUU.HAMNAZO HAYAWANI,SIKILIZA IMELALAMIKIWA MIKOA MINNE TUU,VIONGOZI SABA TUU.TANZANIA INA MIKOA 30 VIONGOZI 60.SIJUI UNAELEWA MCHIZI.HILO MOJA.PILI JEE UNAMJUA CHIKU GALAWA? UNAMUELEWA MECK SADIKI?HAWA NI VIONGOZI MAKATILI KUPINDUKIA.HII MIDOMO MICHAFU KAMA WAKO IKO SIKU TUTAANZA KUIPELEKA POLISI,MFUNGWE.
Ukawa wacha walie tu lakini haitawasaidia maanake wananchi wameshaamua. Hapa ni kazi tu na Magufuli ni rais wetu wa awamu ya tano.
Post a Comment