ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 16, 2015

DKT SHEIN AMNADI DKT MAGUFULI KISIWANI UNGUJA LEO,ASEMA ANATOSHA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein akimnadi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli mbele ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.

Dkt Shein emebainisha wazi kwenye mkutano huo wa kampeni kuwa Dkt Magufuli ni mtu sahihi na anatosha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,amesema kuwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano atashirikiana nae kwa kila jambo kuhakikisha Tanzania inapiga hatua zaidi kimaendeleo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.PICHA  ZOTE NA MICHUZI JR-KISIWANI UNGUJA.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Kisiwani Unguja na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja mjini humo,ambapo Mgombea Urasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufui aliwahutubia.

Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein akimsikiliza kwa makini Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli kabla ya kupanda jukwaani na kuwahutubia maelfu ya wakazi wa kisiwani Unguja kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani humo.
Wananchi wa kiswani Unguja wakishangilia jambo kwenye mkutano huo wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mh Al Hassan Mwinyi  akiwahutubia Wananchi (hawapo pichani) ,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini,Ndugu Boraafya Silima akizungumza machache kwenye mkutano wa kampeni kabla ya kumkaribisha Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kuwahutubia wananchi wa kisiwani Unguja.
Nyomi la wakazi wa Kisiwani Unguja ndani ya mkutano wa kampeni.
Sehemu ya umati wa wakazi wa kisiwani Unguja na vitongoji vyake wakiwa  wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.
Baadhi ya Wafuasi wa chama hicho wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
Wadau wakifuatilia mkutano wa kampeni ndani ya uwanja wa Mnaji Mmoja kisiwani Unguja.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mh Al Hassan Mwinyi  akiwahutubia Wananchi (hawapo pichani) ,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.

wakifuatilia mkutano wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwapungia wananchi wa Kisiwani Unguja (hawapo pichani),alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Mnazi Mmoja mjini humo.
Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia wananchi wa Kisiwani Unguja kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja.


Baadhi ya Wafuasi wa chama hicho wakifurahia jambo kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
Sehemu ya umati wa wakazi wa kisiwani Unguja na vitongoji vyake wakiwa  wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.
Wananchi wa Kisiwani Unguja wakifuatilia mkutano wa kampeni ndani ya viwanja vya Mnazi Mmoja.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimtambulisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa wananchi na wanaCCM wakati alipokuwa akimuombea kura katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM Uliofanyika leo Uwanja wa Mnazi Mmoja Mjini Unguja.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa  visiwa vya Unguja kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisisitiza kuulinda Muungano na kuwaambia kuwa atazifanyia kazi kero zilizobaki za Muungano.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Sheinakihutubia wakazi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.
 Makamu wa Rais wa Dk.Gharib Bilal akihutubia wakazi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaombea kura Dk. John Pombe magufuli pamoja na Dk. Ali Mohamed Shein.
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Hassan Mwinyi akihutubia kwenye mkutano wa kampeni zakuwanadi wagombea wa nafasi za urais kupitia CCM .
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kabla ya kuhutubia wananchi na wanaCCM waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM Uliofanyika leo Uwanja wa Mnazi Mmoja Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kabla ya kuhutubia wananchi na wanaCCM waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM Uliofanyika leo Uwanja wa Mnazi Mmoja Mjini Unguja.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Sheta akitoa burudani kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Mnazi Mmoja.






1 comment:

Anonymous said...

Ukawa umetiwa jiti umedhibitiwa, haufurikuti Zanzibar. Hiyo ni tafsiri rahisi kabisa ya hilo kawa lilotundikwa hapo juu ya mti. CCM inawenyewe na wenyewe ni wanzanzibari. Hakuna cha kafu au ukawa CCM Zanzibar lazima itashinda uchaguzi.