ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 21, 2015

KINANA AMNADI NAMELOK SOKOINE KATA KWA KATA MONDULI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Moita ambapo alimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Monduli Ndugu Namelok Sokoine pamoja na Diwani wa kata hiyo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Moita ambapo alimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Monduli Ndugu Namelok Sokoine pamoja na Diwani wa kata hiyo.
Katibu Mkuu ameendelea pia kumuombea kura mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli na kumueleza ni kiongozi mchapakazi na penda maendeleo.

Mgombea Ubunge jimbo la Monduli kupitia CCM Ndugu Namelok Sokoine akinadi sera za Chama Cha Mapinduzi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Moita.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiwasili kata ya Monduli Juu akiongozana na mgombea ubunge wa jimbo la Monduli Ndugu Namelok Moringe Sokoine .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Viongozi wa Wamaasai (Ole Guanan) wa Monduli Juu.
 Mgombea ubunge jimbo la Monduli akiomba kura kwa wakazi wa Monduli Juu mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo CCM inaomba kura za nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na Ma Ole Guanan wa Monduli juu mara baada ya kumaliza kumnadi mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli, mgombea ubunge Ndugu namelok Sokoine na Madiwani.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Naalarami ambapo alimnadi Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Mgufuli ,mgombea ubunge wa jimbo la Monduli ndugu Namelok Sokoine na Diwani
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili nyumbani kwa Waziri Mkuu Marehemu Edward Moringe Sokoine ambapo alitembelea kaburi alipozikwa Waziri Mkuu huyo.
 Kaburi la Marehemu Edward Moringe Sokoine.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kata ya Mto wa Mbu.
Mgombea Ubunge jimbo la Monduli kupitia CCM Ndugu Namelok Moringe Sokoine akihutubia wakazi wa kata ya Mto wa Mbu waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni,kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye ameendelea kufanya mikutano ya kampeni kwa nafasi ya urai, wabunge na madiwani wa CCM.





5 comments:

Anonymous said...

Watu kiduchu chezea Lowassa wewe
Monduli ni Lowassa

Anonymous said...

hapa ndiyo balaa...huyu binti kapewa hii kiti from lowassa now ccm wanampigia kampeni....ndiyo kuchanganywa......

Anonymous said...

Mkumbuke hadithi ya David and Goliath. Msimdharau huyu binti kkwa kutishika na jina la Fisadi wenu. Tarehe 52/10/2015 atawashangaza.

Anonymous said...

pole binti sokoine.kwenye uchaguzi huu ukipata kura 200 uje ufanye sherehe kubwa mno hapo nyumbani kwenu.na mimi uje unialike.naitwa basilati muuza samaki wa babati-hanang.

Anonymous said...

Hakuna kudanganywa hapa. Kumbukeni hadithi ya David na Goliath. David kijana mwenye umbo dogo aliliangusha dume lenye miraba minne na akapongezwa kwa ujasiri wake huo. Hivyo Namalek Sokoine asitishwe na hawa wanaojiona wenyewe kuwa wababe. Siku yao ya mwisho imefika.