Friday, October 23, 2015

LOWASSA AENDELEA NA KAMPENI ZAKE LEO RUAHA

 
Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa akiongea na wananchi wa Ruaha katika viwanja vya Tem K2 Ruaha leo Ijumaa 23/10/2015
 Mgombea ubunge wa jimbo la Mikumi Joseph Haule akimueleza matatizo ya Mikumi Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa pamoja na kuzungumza na wananchi waliofika katika viwanja vya Tem k2, leo Ijumaa 23 Oktoba 2015
Wananchi wakishangilia katika mkutano huo
Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa pamoja na Mhe. Fredrick Sumaye wakiwasili katika viwanja vya Tem K2 Ruaha, leo Ijumaa 23/10/2015.

5 comments:

Anonymous said...

huu ndio uhalisia wa mapokeo ya watanzania kwa kiongozi ambaye mioyo yao imekunwa naye,kiongozi asiye shaka,mwanamume wa shoka,anayelindwa na watanzania wenyewe huku akifanyiwa kila njama,kiila aina ya faulo ambayo binaadamu unaijua ili kupunguza kasi yake ya uungwaji mkono kitu ambacho kwa tanzania na hawa watanzania wa leo haiwezekani. kumhujumu,ni sawa na kuwahujumu wapiga kura wenyewe na si lowassa.MFANO WA HUJUMA KUBWA NI LEO IJUMAA TAREHE 23 OCTOBA 2015 KUANZIA SAA 3 USIKU MHE.LOWASSA ALIKUA ANAONGEA NA TAIFA KWA NJIA YA TELEVISHENI NA REDIO GHAFLA TUU ILIPOFIKA SAA 3 DAKIKA 2O TANESCO WAKATUMWA KUUZIMA UMEME WOOTE WA GRID.UMEME UMERUDISHWA SAA 7.05 USIKU. MAMILIONI TUMEKOSA KUMSIKILIZA MHE.LOWASSA KWA NJAMA NA HUJUMA HII MBAYA. IKUMBUKWE LEO CCM WALIKUA WANAFUNGA KAMPENI ZAO JANGWANI,REDIO NYINGI,VITUO KADHAA VYA TV WALIKUA HEWANI TANGU SAA 2 ASUBUHI HADI SAA 1 USIKU,UMEME HAUKUKATIKA HATA CHEMBE.mnataka nini ccm,mnazidi kuwatia hasira raia na majibu yapo jumapili tarehe 25 octoba 2015 kwenye masanduku ya kupigia kura.MWENYEZI MUNGU YUPO UPANDE WETU RAIA TULIOKWISHAAMUA KULETA MABADIRIKO NCHINI.

Anonymous said...

Ilani ya Ukawa " mnanionea "...

Anonymous said...

Mimi namkubali Lowassa kuwa ni mkweli na sio mtu wa kupayuka.kwasababu siasa ni kuleta maendeleo kwa wananchi sio matusi wala kejeli. Pia nitampigia kura kutokana ataileta katiba ya Warioba ambayo sisi wananchi ndio itatutoa shimoni. Hebu angalia leo mtu unafanya kazi bila mkataba na tajiri anakutuma mambo yasiokuwa ya kikazi lakini utafanya kutokana hutaki kuikosa kazi yako. ndio sawa na wananchi hatuna katiba ndio maana ccm wanafanya watakavyo, na kuiba watakavyo sisi mlo mmoja kazi kuupata yaani mtu unakaa unajiuliza leo nitakula nini tumbo utasema lina chura huku viongozi wanakula milo mitano mpaka vyengine wanavimwaga.nikitakacho mimi ni katiba itakayoleta heshima kwa wananchi na viongizi wakikosea ili tuweze kuwajibisha na kuwa mwisho wa ufisadi.

Anonymous said...

ILAANI YA CCM,"MKISHAPIGA KURA RUDINI NYUMBANI MKALALE,MATOKEO MTATANGAZIWA NA JANUARI MAKAMBA WA CCM,HIYO JUMAPILI TAREHE 25 OCTOBA 2015 SAA 7 USIKU".

Anonymous said...

Chaguo la rais kwa Watanzania wengi ni Magufuli.