Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akilakiwa na wananchi wa Jimbo la Monduli wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Barafu, Mto wa Mbu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni, leo Oktoba 2, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Babati Mjini, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kwaraha, Babati Mkoani Manyara leo Oktoba 2, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Monduli, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu, Mto wa Mbu, leo Oktoba 2, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli wa Chadema kupitia mwamvuli wa UKAWA, Julius Karanga, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu, Mto wa Mbu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni, leo Oktoba 2, 2015.
5 comments:
mimi niikuwepo katika mikutano yote mitano ya mheshimiwa lowassa alipokua na sisi wenyeji wa dar-es-salaam juzi alhamisi tarehe 1 octoba 2015.leo hii hatujadiri umati wa wahudhuriaji kama ilivyo pichani,ni malaki kwa malaki,na kazi zooote husimama na nikiendelea kufuatilia mazungumzo ya wananchi mbali mbali wa hapa dar-es-salaam na pia kwa upande wa pili kuona na kushuhudia hamasa za wanachama sugu wa ccm kujibu mapigo yaani uhudhuriaji wao wa mikutano ya ccm kampeni inayoendelea.aaah,kwa jina la mungu,na ninawaambieni sitanii,ccm wameelemewa tena,wameelemewa vibaya sana kwa mbali mno mno.hilo sasa wenyewe wanalijua na mzigo wooote wa lawama wanamuelekezea mtu mmoja tuu,mheshimiwa jakaya mrisho kikwete mwenyekiti wa sasa wa ccm.wanasema chuki zake binafsi na za wazi kwa mheshimiwa edward lowassa`ndizo ambazo sasa dhahiri zimeiondoa ccm kutoka chama-dola mnamo siku ya jumapili tarehe 25 octoba 2015 hadi chama kipya cha upinzani.wanafika mbali kujiuliza jee ccm inapoingia hali hiyo mpya ya kisiasa ambayo haijawatokea kwa miaka 55 jee watasalimika kubaki kama chama ccm?sasa hivi wapenzi wa ccm robo tatu ni akina mama wanakwenda na sare zao kwa kificho kwenye mifuko wakifika kwenye arena wanavaa.mkutano ukiisha wanavua tena sare zao kwenye mifuko wanasambaa.hii ndiyo hali halisi ya dar-es-salaam
Tunajua Chadema na Ukawa yenu mmepitia chuo cha uongo na uongo kama huu unaoutoa hapa utaendelea kuwaridhisha upande wenu tu kwani mambo unayofikiria kuwa ndiyo, sivyo. CCM na wanachama wake hata kidogo hawawezi kumlaumu Kikwete na wajumbe wengine kwa kumtosa Lowassa. Sana sana wanashangilia kitendo hicho kwani huyu mtu wenu alikuwa ni mzigo mkubwa sana kwa chama tawala na nyinyi mnajua. Kunyanyuka kwenye chati kwa Chadema na Ukawa kwa ujumla unatokana na mashambulizi yenu makali kwa Lowassa na CCM kuwa walikumbatia kwa vitendo vya ufisadi. Kama Lowassa na wenzake wasingeondoka, CCM ilikuwa mashakani sana kwenye uchaguzi mwaka huu kwani kitendo cha ufisadi kingeendelea kuwanyanyasa na kuwafanya wasipate usingizi mnono kutokana na kuwa kitendo cha ufisadi ni kitendo ambacho watu wengi wanakichukia na hawataki hata kukisikia. CCM sasa imepumua kwani mafisadi wamekimbilia Chadema na Ukawa vyama ambavyo sasa zinapambana na joto la wananchi. Ukitilia maanani haya yote hakuna sababu yoyote ya kuwafanya akina mama wa chama tawala kuficha sare zao wanazojivunia. Huo ni uongo wa hali ya juu na tarehe 25/10/2015 yote yatawekwa bayana. Mwandishi wa habari usijifiche kwani tutapenda sana kusoma hoja zako kwenye blog hii baada ya uchaguzi.
Tunajua Chadema na Ukawa yenu mmepitia chuo cha uongo na uongo kama huu unaoutoa hapa utaendelea kuwaridhisha upande wenu tu kwani mambo unayofikiria kuwa ndiyo, sivyo. CCM na wanachama wake hata kidogo hawawezi kumlaumu Kikwete na wajumbe wengine kwa kumtosa Lowassa. Sana sana wanashangilia kitendo hicho kwani huyu mtu wenu alikuwa ni mzigo mkubwa sana kwa chama tawala na nyinyi mnajua. Kunyanyuka kwenye chati kwa Chadema na Ukawa kwa ujumla unatokana na mashambulizi yenu makali kwa Lowassa na CCM kuwa walimkumbatia kwa matendo ya ufisadi. Kama Lowassa na wenzake wasingeondoka, CCM ilikuwa mashakani sana kwenye uchaguzi mwaka huu kwani kitendo cha ufisadi kingeendelea kuwanyanyasa na kuwafanya wasipate usingizi mnono kutokana na kuwa kitendo cha ufisadi ni kitendo ambacho watu wengi wanakichukia na hawataki hata kukisikia. CCM sasa imepumua kwani mafisadi wamekimbilia Chadema na Ukawa vyama ambavyo sasa vinapambana na joto la wananchi. Ukitilia maanani haya yote hakuna sababu yoyote ya kuwafanya akina mama wa chama tawala kuficha sare zao wanazojivunia. Huo ni uongo wa hali ya juu na tarehe 25/10/2015 yote yatawekwa bayana. Mwandishi wa habari usijifiche kwani tutapenda sana kusoma hoja zako kwenye blog hii baada ya uchaguzi.
Sema ni uongo lakini ukweli utajidhihirisha siku siyo nyingi. Ukweli unaonyesha jinsi ambayo ccm imejichokea ni kutumia pesa ovyo kuhamisha watu na malori. Mbio za sakafuni.
Mtaona ukweli tarehe 25/10/2015 wakati CCM itakapo chukua madaraka tena.
Post a Comment