Advertisements

Wednesday, October 7, 2015

LOWASSA AWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA AJIRA ZITOLEWAZO NA AFRIKA MASHARIKI

WATANZANIA wametakiwa kujifunza kuchangamkia fursa za ajira zinazotolewa na Afrika Mashariki kama ilivyo kwa nchi nyingine.

Kauli hiyo ilitolewa jana na mgombea wa Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa alipokuwa kwenye kampeni zake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Namanga.

Lowassa alisema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atahakikisha kuwa watanzania wanachangamkia fursa za Afrika Mashariki kama ilivyo kwa Kenya.

"Napenda mahusiano ya Afrika Mashariki yawe ya kweli na siyo upande mmoja unafaidi na mwingine haufaidi,"alisema na kuongeza kuwa:

"Watanzania wakiwa wanapita kwenye mpaka wa Namanga wasisumbuliwe wapite bila shida."
Sehemu ya wananchi wa eneo la Kisongo, Jijini Arusha wakiwa wamefunga barabara kuzuia msafara wa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, ili waweze kumsalimia na kumsikiliza, wakati alipokuwa njiani kuelekea eneo la Ngaramtoni mpaka Namanga, kwenye Mkutano wa Kampeni, leo Oktoba 7, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, ARUSHA.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwa vijana wa eneo la Kisongo, walipokuwa wakimsindikiza mpendwa wao.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Mringa, Jimbo la Arumeru Magharibi, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Jimbo la Arumeru Magharibi waliohudhulia Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Mringa, Jimbo la Arumeru Magharibi, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Arumeru Magharibi katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Mringa, Jimbo la Arumeru Magharibi, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Jimbo la Longido waliohudhulia Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa Namanga, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwasalimia watoto walikuwepo kwenye Mkutano huo.
Lowasaaaaa......   Mabadilikoooooooo......
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwasalimia wananchi wa Mji wa Namanga, katika Jimbo la Longido, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Namanga, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Namanga, Jimbo la Longido, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Namanga, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015. 
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido kupitia Chadema, Onesmo Ole Nangole, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Namanga, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015. 
Zawadi: Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akionyesha kwa wananchi zawadi iliyotolewa na Vijana wa Mji wa Namanga kwa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa.
Burudani ya Asili ya Kimaasai.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiteta jambo na aliewahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani katika Serikali ya Kenya, Mzee John Keen, aliefika eneo la Namanga kuhudhulia Mkutano wa Kampeni zake, leo Oktoba 7, 2015.









4 comments:

Anonymous said...

ASANTE MKOMBOZI WETU MHESHIMIWA LOWASSA.PANDE LA PASHO LA KWANZA KWA NCHI MAJIRANI ZETU ANASEMA MHESHIMIWA LOWASSA,TUNAUPENDA SANA USHIRIKIANO,LAKINI USHIRIKIANO HUU USIWE WENYE FAIDA KWA UPANDE MMOJA HAPANA,WITH BIG NO,KWA MAANA NYINGINE TANZANIA ISIGEUZWE KOLONI LA UCHUMI LA NCHI JIRANI,HAPANA.MIMI NIFAIDI NA WEWE UFAIDI HII NDIYO FORMULAR YA UJIRANI MWEMA.KIKWETE AMEUHARIBU SANA UWIANO WA BIASHARA NA UCHUMI LINGANIFU BAINA YA TANZANIA NA KENYA,KWA MAANA NYINGINE KIUCHUMI,TANZANIA NI MKONO MREFU WA KENYA.WANATUTAWALA KWA KUFYONZA KILA TULICHOKUA NACHO.JUZI KIKWETE KAMUAGA KENYATTA ANAMUHAKIKISHIA KWA KUWA [ANAONA]ATAENDELEA KUWA REMOTER WA KIG'AMUZI MAGUFULI AMBAYE NAYE BAHATI MBAYA ZAIDI NI RAFIKI WA DAMU WA MWANASIASA RAILA OGGA ODINGA WA KENYA,KWAMBA HAPATAKUA NA MABADIRIKO YA TRADE AND ECONOMIC IMBALANCE HILI[UKISIKIA KUNUNULIWA NDIKO HUKO]KWA MHESHIMIWA LOWASSA HALIPO.EWE MWENYEZI MUNGU UZIDI KUMPA UJASIRI NA KUMUANGAZIA KIPENZI CHA WATANZANIA MHESHIMIWA LOWASSA TUMPE NCHI,ATUKOMBOE,TUMEUMIA SANA KIUCHUMI.

Anonymous said...

Tangu lini Magufuli akawa rafiki wa damu na Raila O. Odinga. Umesahau kuwa Lowassa ndiye rafiki wa Odinga na juzi tu wakati mnafungua kampeni zenu za kuwania urais hapo Jangwani, Dar es Salaam, mlimkaribisha Odinga kama mgeni wenu. Hili ndiyo tatizo la kukurupuka kuandika bila ya kufanya utafiti wa yale mnayoandika.

Anonymous said...

UNASEMA NINI CHIZI WEWE UMESAHAU NA USIUPOTOSHE UMMA RAILA OGINGA ODINGA NI RAFIKI MKUBWA SANA WA JOHN MAGUFULI.NINA HAKIKA KICHWA CHAKO NI, KAMA SIO KICHAFU NI KIBOVU.KAMATA HILI.MARA TUU BAADA YA MAGUFULI KUPITISHWA NA CCM KAMA NDIYE MGOMBEA WAKE RASMI WA URAIS MNAMO JULY KATI 2015 MGENI WAKE WA KWANZA KUTOKA NJE YA TANZANIA KUFIKA KUMPONGEZA KWA USHINDI HUO ALIKUA NI RAILA ODINGA KUTOKA KENYA AKIAMBATANA NA MKEWE.PIA NAKUKUMBUSHA NI HUYU HUYU MAGUFULI WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU WA KENYA MIAKA MINNE ILIYOPITA ALIWAHI KUSAFIRI MPAKA KENYA KUMPIGIA KAMPENI RAFIKI YAKE RAILA ALIPOKUA ANAGOMBEA URAIS.WATU MBALI MBALI NA VYOMBO VYA HABARI WALIMLAANI SANA MAGUFULI KWA KUINGILIA SIASA ZA NDANI ZA KENYA. HIVI WEWE MBONA MJINGA HIVI,UNAKANUSHA NA HILO?HEBU ONDOA UVUNDO WAKO.

Anonymous said...

Matusi yako hayasaidii na wala huwasaidia wana Ukawa wenzio kwani kwa lugha yako watu watafikiri kila mmoja kwenye chama hiki anapenda kutukana kumbe sivyo.