Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mchungaji Maboya mmoja wa viongozi walioshiriki Tamasha la kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na maaskofu na wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili kutoka Tanzania na nje ya nchi kwenye Tamasha la kuombea Amani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 lililofanyika kwenye uwanja wa Taifa hapa Dar es Salaam tarehe 4.10.2015.
Mamia ya wananchi waliohudhuria Tamasha la kuombea amani kuelekea Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 wakifuatilia wasanii mbalimbali wa nyimbo za injili waliokuwa wakiburudisha kwenye tamasha hilo lililofanyika kwenye uwanja wa Taifa tarehe 4.10.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi waliohudhuria Tamasha la kuombea Amani kwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwenye Uwanja wa Taifa tarehe 4.10.2015. Anayepunga mkono kushoto ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Wasabato Tanzania ndugu Mark Warwa Marekana.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipeana mkono na Askofu Mkuu wa Kanisa la Wasabato Tanzania Ndugu Mark Warwa Marekana mara baada a Mama Salma kuwasili kwene uwanja wa Taifa ambapo alimwakilisha Rais Dkt. Kikwete kwenye tamasha hilo.
Mke wa Rais ,Mama Salma Kikwete akipokea Tuzo Maalum kwa niaba ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Wasabato Tanzania Ndugu Mark Warwa Marekana wakati wa Tamasha la la kuombea Amani kwenye Uchaguzi Mkuu ujao
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa album mpya ya Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Ndugu Ben Mwaitege wakati wa Tamasha la kuombea Amani kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015 lililofanyika Uwanja wa Taifa hapa Dar es Salaam tarehe 4.10.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria Tamasha la kuombea Amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 lililofanyika kwenye Uwanja wa Taifa tarehe 4.10.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi mbalimbali waliohudhuria Tamasha la kuombea Amani kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015 lililofanyika kwenye Uwanja wa Taifa tarehe 4.10.2015.
3 comments:
Mbona mama Salma Kikwete ameruhusiwa kuutumia huu uwanja kwa shughuli za kisiaasa? Sio majuma mawili au matatu tu yamepita waliowanyima UKAWA kutumia uwanja huu wamesahau? Jamani TANZANIA ni nchi ya watu fulani fulani? Eh Mungu irehemu na utusamehe makosa yetu!
Huu siyo mkutano wa chama chochote na wala siyo kampeni za uchaguzi. Usingekuwa na papara katika kusoma yaliyoandikwa ungeona kuwa mjumuiko huu uliandaliwa kwa ajili ya Watanzania wote, wapenzi wa vyama vyote, waumini wa dini zote na kila Mtanzania anayependa amani ili waliombee taifa letu liwe na amani wakati huu tunaoelekea kwenye uchaguzi na baada ya uchaguzi.
UNAJUA ALEX MSAMA ULIYEKUWA MWANDAAJI WA TUKIO HILI MUHIMU LILILOKUWA LINAPASWA KUHUSISHA SALA NA MAOMBI,NA UKICHUKULIA MAANANI KIPINDI HIKI TUNAPOELEKEA UCHAGUZI MKUU HAPO 25 OCTOBA ZIMEBAKI SIKU 18 TUU NA KAMA ULIKUA NA MAANA YA DHATI YA KWELI KULIOMBEA AMANI TAIFA LETU,BASI WALENGWA WAKO WAKUU WANGEKUA VIONGOZI MBALI MBALI WA MADHEHEBU NA DINI ZOTE NCHINI MGENI RASMI NINI KATIKA HILI.HAO NDIYO WATOA SALA,MAOMBI,DUA NA HAO NDIYO DIRA YA AMANI YA NCHI,ILIYOPO NCHINI.BAHATI MBAYA KWA KUELEWA AU KWA KUTOKUELEWA ULIMTANGULIZA MWENYEKITI WA CCM WA TAIFA MHE.JAKAYA KIKWETE KIUSHABIKI ILI AWE MGENI RASMI KWENYE TAMASHA LILE.IT WAS A COMPLETE FLOP KWANI MHESHIMIWA ALIKUA NA ANOTHER OFFICIAL ENGAGEMENT KENYA NA AKAMTUMA MKEWE KUMUWAKILISHA KWA HIYO ULIWATAPELI WAHUDHURIAJI.TAMASHA HILI HAKUPASWA AALIKWE KIKWETE AMBAYE MOYO NA MAWAZO YAKE YOTE KWA SASA NI KUIPIGIA KAMPENI CCM ISHINDE.KWA MAANA NYINGINE WEWE MSAMA NI KADA WA CCM ULIYEKOSA HEKIMA NA AKILI YA MPAMBANUO WA NYAKATI,NA UKAANGUKA.TULIONA,TUKASEMA NGOJA TUONE,UMELETA FEDHEHA NA KUTIA AIBU.
Post a Comment