ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, October 18, 2015

MDAHALO WA WAGOMBEA URAIS TANZANIA WAFANYIKA, MAGUFULI, LOWASSA WASHINDWA KUHUDHURIA

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Nghwira (kulia), na Mgombea nafasi hiyo kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chifu Litayosa Yemba wakijibu maswali mbalimbali katika mdahalo wa wagombea urais ulioandaliwa na Taasisi ya Twaweza Dar es Salaam leo. Hata hivyo wagembea nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.John Magufuli na Edward Lowassa kupitia Chadema hawakuweza kuhudhuria kwa sababu mbalimbali.
 Waongozaji wa mdahalo huo wakiwa kazini. 
 Wadau wakiwa kwenye mdahalo huo.
 Raia wa kigeni na wadau wengine wakifuatilia mdahalo huo.
 Mdahalo ukiendelea.
Vijana wakiwa kwenye mdahalo huo.


Na Dotto Mwaibale



MGOMBEA wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John  Magufuli pamoja na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), pamoja na vyama vinaunda Ukawa, Edward Lowassa leo wameshindwa kuhudhuria mdahalo maalumu wa wagombea urais ulioandaliwa na mkimkiki kutokana na sababu mbalimbaliu.



Mdahalo huo ulikuwa unajadili mambo mbalimbali kama vile uchumi,katiba ya uchaguzi,malengo endelevu ya umoja wa mataifa, katiba inayopendekezwa, viashiria vya uvunjifu wa amani nchini,uchumi na huduma za kijamii kwenye sekta ya afya.



Wakizungumza kwenye mdaharo huo Dar es Salaam wagombea nafasi za urais kupitia vyama vya ACT-wazalendo, ADC na TLP walikuwa na mengi ya kuelezea kuhusu mstakari wa taifa la Tanzania. 



Mgombea urais wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chief Lutasola Yemba akijibu swali lilioulizwa kwamba wagombea hao watawezaje kuondoa rushwa kwa wanafunzi pindi wanapotafta ajira endepo akipata ridhaa ya kuingia madarakani alisema. 



SWALI  

Mtawezaje kuondoa tatizo la rushwa kwa wanafunzi waliokoswa nafasi za kazi kwa maadai ya kukoswa uzoefu huku wakiombwa chochote kabla ya kupewa ajira rasmi.


Chief Yemba alisema Serikali ya ADC itahakikisha wanafunzi wanatakiwa kupata kazi punde baada ya kuhitimu masomo yao bila kusubiri kupata uzoefu huku akiwa anafanya kazi katika taaluma yake hata kama ni kwalipo kidogo na kwa baadae atakuwa na uzoefu mkubwa.



Kwa upande wake mgombea urais kupitia Chama cha  ACT- wazalendo ,Anna mghira akijibu swari hilo alisema rushwa ni utamaduni lakini chama cha ACT- wazalendo kiatatoa elimu ya rushwa tangu wakiwa wadogo,ambapo itakuwa ni utamaduni wa mwanafunzi tangu akiwa mdogo.



''Pia tumeweka mikakati ya utekelezaji ambapo ni namna tutakavyoshughulika na mikakati mbalimbali huku tukiwajumlisha wananchi kutoa maoni yao na kurudi kwetu kiutekelezaji ili kuziba mianya ya rushwa ,''alisema



Swali

Nini tofauti kati ya ugonzi na mfumo wa uendeshaji wa Serikali yaani utawala?


Mghira alisema Chama hicho kitahakikisha kinashirikiana na watanzania katika suala zima l;a uongozina  kuongoza kwa uhuru huku akisema utawala ni kuendesha watu kwa kutoa amri na masharti bila kujali.



Kwa upande wake Chief Yemba akijubu swari hilo alisema kupitia chama cha ACT wazalendo tutahakikisha tunawashirikisha wananchi kila jamabo ili kuwa viongozi ambao wanashirikiana na wananchi wake na kufikia maendeleo kwasababu sisi hatutaki kutawala wananchi bali  kuwaongoza watanzania,''alisema.



Sifa za kuwa Rais



Mghira Naielewa nchini yangu vema,mimi nimwanasheria kitaluuma ni elimu inayoweza kumleta mtu kumudu kuishi pamoja na kushughulikia migogoro ya jamii



''Nikichanganya na hii ya elimu ya haki za binadamu naamini kabisa naweza kuwa Rais wa nchi na upole wangu sio udhaifu,upole ni nguvu na naweza kuwatumikia watanzania na kuwa kiongozi wao mzuri,''alisema.



Alisema Taifa lilipofikia kwa sasahivi linahitaji mtu anae weza kutatua migogoro kwa njia ya busara na si kupiga kelele na upole wangu ni nguvu kwa taifa hasa katika wakati huu abao taifa linaonekana kuwa katika mgongano.



Chief Yemba alisema Urais hauna uzoefu wala mtu asiseme mimi siwezi kwasababau uraisa ni tasisi na hakuna mtu anaeweza kuwa Rais peke yake bila kushirikiana na wezake mimi ni rais bora wa Tanzania.



''Nimekuwa Rais wa klabu za soka katika kipindi chote cha maisha yangi tangu mwaka 1886 na sasa nimeteuleiwa na chama changu kuongoza ilani ya chama ili kufikia mafanikio ya kuondoa umasikini maradhi na ujinga,''alisema.



Alisema amekuwa mfanyakazi bora katika kipindi chote alipokuwa nikifanya kazi katika klabu za mpira na amekuwa akiibua vipaji vya wachezaji pia hajawahi  kufanya kazi bila mafanikio kwa wananchi.



Kukomesha rushwa



Mghira Rushwa ni tatizo kubwa katika taifa letu,mimi nitashughulikia kuondoa mazingira magunu kazini,kuboresha mazingira ya kazi ili kuwafaya wafanyakazi kuwa huri.



Alisema Atajitahidi kuweka sera katika utumishi wa umma kuweza sheria na taratibu ambazo zikifuatwa zinaweza kuondoa tatizo la rushwa nchini.



''Taifa linahitaji kuwa na ukusanyaji wa mapato wa kutosha kutoka asilimia 11 ya sasa na kufikia asilimia 25 kama chama changu kilivyojipangia pamoja na kuzibiti kodi katika ukusanyaji na kuziba mianya ya ukusanyi kodi na hapo tutapa mapato yanayopotea,''alisema.



Tume ya uchaguzi.



Mghira alisema kitendo cha watu kuambiwa wakishapiga kura warudi nyumbani hii ni hali inayoonesha tume haipo huru kwaababu kama ingekuwa huru isingefanya hivyo, lakini labda nikwasababu bado tunatumia utaratibu wa tume ya zamani.



''Naaiamnini na ningeomba watende haki katika kipindi hiki ili kutoa haki kwa wagombea wa nafasi mbalimbali katika mchakato huu,''alisema.



Chief Yemba tume naaimani lakini haipo huru kwasababu ya mfumo wa kiutawala unaingiliana na chama tawala kwa asilimia kubwa haifanyi mambo yake kama tume,pengine utasikia kamuli mbalimbali laini tume haitoa onyo.



Uzalendo



Chif Yemba alisema uzalendo ni hari ya kujitoa katika kulitumikia taifa na kuhakikisha kwamba wanalililetaea taifa faida na si hasara, na kwamba kama atapata ridhaa ya kuwa Rais wa nchi atashirikiana na chama chake kuweka misingi ya  umoja ustahimilivu,uwajibikaji,ushirikishwaji na maadili ya uongozi ambayo yatasaidia kuondoa ufisadi.



Mghira alisema yeye akiingia madarakani kama atapa ridhaa anataka kuweka uzalendo kwanza kwenye usambazaji wa habariili kutoa fursa pana na uhuru wa habari nchini.



''Mimi naamini katika kutoa habari na kuzisambanza kwa wanachina hili likpokatika ilani ya chama changu ambapo tuatahakikisha wanahabari wanakuwa huru kutafta habari na kurejesha kwa wananchi,''alisema.




Chief Yemba alisema yeye anaamini katika ushirikishwaji wa wananchi katika mambo mbalimbali yanayofanyiwa tafti kwajili ya maendeleo ya Taifa na pia ,chama chake kinaamini katika tafti za kisayansi.



''Suala la sheria ya makosa ya mtandao ni zuri lakini inabidi kuangaliwa ili kutowabana wanahabari kutoa habari kwa wananchi kwasababu taifa bila habari ni taifa lilokufa,''alisema. 




Msimamo wao katika katiba pendekezwa.



Yemba mimi sisemi kama kuna katiba mpya bado tunatumia katina ya zamani maana hata ile anayosemwa imefanyiwa marekebisho lakini bado haijafika kwa wananchi.



Alisema kama atapata ridhaa ya wananchi kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano atahalkikisha mchakato wa katiba unarudiwa upya na pia kwenda kwenye tafti kuangalia katiba ya jaji waryoba kama inakidhi vigezo kama la wataongeza vipengere vya msingi.



Mghira alisema akam atapata ridhaa ya kuwa Rais wa Tanzania kwa wamu ya tano atahakikisha chakato wa katiba unarejeshwa kwasababau mchakato huo haukukubalika na wananchi mwanzoni.



Swali

Viashiria vibaya vya mgawanyiko ambayo vinajitokeza,hali hii mnaionaje na mkiingia madarakani mtaikomeshaje.


Chief Yemba tatizo kubwa linaletwa na watu wanaofikiri tumbo badala ua watu,ili kuondoa viashiria hivi inabidi kupata mtu ambaye anaangalia watu na si utu wala tumbo lake.



''Tutahakikisha tunaondoa misngi ya viashiria kwa misngi ya haki katika dini zote na kutokuwepo kwa ukanda,nawashauri watanzania kuchangua ADC kuondoa tofauti,''alisema.



Mgwilla akijubu swali hilo alisema anafuriki ubaguzi upo kwa viongozi zaidi kuliko wananchi,japo yeye hakukutana na ubaguzi wa aina yeyote katika kupita huko na kule kwenye kampeni zake.



''Mwanzoni nilikuwa na fikra za kukutana na ubaguzi kwasababau katika Taifa letu kuna kawaida ya kumkubali mwanamume kwa kila kitu anachokifanya lakini si mwanamke,namshukuru Mungu sikukutana na ubaguzi wa aina yeyote walifrahi kuniona na wamenikubali,''alisema.



Muungano



Mghira akizumngumza kuhusiana na muungano alisema   muungano wa tanganyika bado hauna ukubali wa wananchi na kwamba hiyo ni changamoto kubwa kwani wananchi wahana ridhaa ya muungano kikatiba hali inayofanya wananchi wa pande zote mbili kugomgana.



Chief Yemba alisema Muungano hauna haki sawa na ili kuwepo na makubaliano ya muungano nilazima haki sawa ipatikane kwa watu wote wa tanzania na Zanzibar,kutoa fursa sawa kwa wote kiuchumi na hata katika sekta ya afya na sekta zingine.



''Tunatakiwa kufikiria kuwa na fursa sawa ili kuondoa malalamiko pamoja na kuwa na mfumo wa Serikali unaopendekezwa na pande zote mbili,''alisema  Chief Yemba.



Mabadiliko ya kweli nchini



Yemba alisema mafanikio ya ADC ni kujikita katika kuondoa ujinga umasiki na maradhi paoja na kuondoa mfumo ambao unafanya kazi katika Serikali ya CCM.



Mghira alisema mabadiliko ya kweli nchini katika Serikali ya  wazalendo ni mtumizi mazuri ya rasilimali za nchi kama vile mafuta gesi na vyanzo vya mapato.



Alisema dhana ya kuiondoa CCM madarakani ni dhana ya   kisiasa lakini CCM yenyewe ingefanya utaratibu wa kuondoka madarakani ili vyama vingine tujaribu kuleta maendeleo katika Taifa hili.



Mapato wanataluuma na wanasiasa.



Watalaam hawapewi mshahara stahiki kama inavyotakiwa,nilazima waboreshe mishahara ya wanataluma,Serikali inatakiwa kutofautisha kulipa mshara wafanyakazi wa kudumu ambao ni watalaamu mkubwa badala ya wabunge ambao ni wana muda mfupi Serilakini.



Chife Yembe Urafiki katika utawala ni tataizo tunachohitaji ni kuwa na mchanganuo mzuri wa kufanya kazi kulingana na taaluma zetu pasipo kuangalia huyo ni rafiki au ndungu maana hii inachangia upendeleo wa mapato kazini katika taluma mbalimbali.





Mghira wanasiasa wanakipato kikubwa kuliko watalaamu kwa sasa lakini sisi chini ya chama changu tutakuza sekta mhimu na kkisha kushughukia sekta za uzalishaji na wanawekeji kuiletea nchi mapato na ttafta posho za wanasiasa ili kuita uwiano wa wanataluma na wanasiasa



''Hakuna uhusiano wa huru unaoonekana kati ya Srikali na Zaki mara nyingi sekta binafsi inakinzana na sekta ya umma,Mimi na chama changu tukiwa tumepewa ridhaa tutaunda kikundi huru ambacho kitashughulikia tatizo hilo ili kuleta mahusiano mazuri kati ya hawa watatu,''alisema Anna.



Uchumi



Mghira alisema ACT tumezungumzia viwanda lakini bado suala hili linachangamoto kubwa kwasababu Tanzania bado hatuna umeme imara na maji ya kutosha katika semunu za vijijini hivyo tutahiji kuweka mikakati madhubuti ya kuweka mifumo rasmi ili kuanza kujenga na kufufua viwanda.



''Mikataba yote itakuwa ya wazi si ya siri ili kuwezesha wananchi kushiriki katika kuisoma na kutoa maamuzi na wale wasioona watapelekewa katika maeneo yao ili kukuza ushrikishaji wa wananchi,''alisema 



Kwa upande wake Chief Yemba alisema ADC wamekubaliana Viwanda vinatakiwa kutokana na wananchi wenyewe huku akitolea mfano wa dhahabu kwamba inatoko chini ya ardhi na mwananchi aliyopo hapo anatakiwa kuwezesha kabla ya kuhamishwa ili kusaidia kuwaendeleza.



TLP



Lazima kuwe na bajeti za kuwesha upanuzi soko la ajira na lazima soko hilo liwashirikishe wazawa yaani wananchi wenyewe na hivyo dhahabu kama ni 2.2 lazima ieleweke kwa wananchi.




Huduma za kijamii kwenye sekta ya afya.

Suala la kujiunga na mifuko ya jamii iwe lazima au hiari.


Mghira Tukifanikiwa kuinua uchumi wa nchi yetui tutweza kuchukua jukumu ya kutoa huduma za afya kwa wananchi bure,na mifuko ya jamii tunaichukulia kama kichocheo cha mapato katika jamii.



Yemba Serikali ya ADC itahakikisha inawaondolea wananchi wake maradhi na ujinga,Serikali itategeneza mfumo wa kumuwekea mwananchi fedha kutoka kwenye rasilimali alizonazo katika eneo lake,hakuna ulazima wa kumlazimisha mwananchi kuchangia huduma za fya.



''Tanzania imejaa rasilimali za asilimi hivyo hakuna sababu ya kumulazimisha mwananchi kulipipa gharama za afya,kinachotakiwa ni kutegeneza mfumo unaotoa fursa kwa wananchi.



Kwanini Hospitali nyingi za umma hazina dawa?



Mghira alisema watapambana na ufisadi kuweka miondombinu imara ili kuhahakisha kuna dawa za kutosha katika hospitali za umma pia dawa zinakosekana kwenye hospitali za umma kukoswa maadili ya kiutabibu.



Chief yemba Kunatakiwa uwajibishaji watu wanaohusika kufanya hivyo wanatakiwa kuwajibishwa na pamoja na kuondoa tabaka la walio nacho na wasio nacho nchini pamoja na kuziba mianya ya rushwa ili kutoa fursa ya kupata matibabu kwa wote  




Tanzania Labour Party(TLP), Macmillan Lyimo akinzungumzia suala la kuisha dawa kwenye hospitali za umma alisema

Lazima mifumo ya ufuatiliaji wa dawa uboreshwe na kuondoa mianya ya rushwa ili kutoa haki kwa watu wanyonge ikiwa ni pamoja na kuwapatia wananchi haki ya kupata matibabu.


Uchumi.



Umejiandaaje kumaliza deni la taifa



Chief Yemba alisema Suala linabakai palepale kuziba mianya ya rusha,lakini tatizo la viongozi wa Tanzania huajibika wakati wa kampeni pekee,ingekuwa vema kama viongozi waliochangia kuingizia nchi deni kubwa wangewajibishwa katika mchakato wa kurejesha fedha,ili kutoa nafasi kwananchi kufanya maendeleo katiik taifa na si kulipa deni kila mwaka.

4 comments:

Anonymous said...

Hauna mshiko

Anonymous said...

Hauna maana ndo maana wenye maana hawakwenda
Shame you

Anonymous said...

LOWASA ALISEMA HATOWEZA KUHUDHURIA KUTOKANA NA UFINYU WA MUDA NA RATIBA YAKE,
MZEE MAGUFULI, NAAHIDI NITAHUDHURIA MDAHALO KWA WAKATI, NA MSIWE NA WASIWASI WALA SIDANGANYI, NINASEMA KWELI TENA KWELI KABISA NA NITASIMAMIAMWENYEWE KWENYE RATIBA "SITAWAANGUSHA" LOWASA KATIMIZA ALICHOKISEMA MAGUFULI AHADI YA KWANZA NA SIMPLE IMEMSHINDA. ATAWEZA?

Anonymous said...

Hapa kazi tu. Wanaotaka kuandika yao na waandike tu lakini tarehe 25/01/2015 ndiyo kikomo na majibu yatatoka.