Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akisalimiana na mmoja wa madiwani waliofika kumpokea mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Singida mjini pamoja na wasaidizi wake.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akiwa ameambatana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Bumbuli, January Makamba ambaye pia ni mmoja wa wanakamati wa timu ya ushindi ya kampeni za Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dk.John Pombe Magufuli, wakielekea sehemu ya mapokezi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Singida mjini.
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akilakiwa kwa furaha na watoto wanaoishi kwenye eneo la uwanja wa ndege Singida mjini.
Watoto wakimpokea kwa shangwe aliyekuwa Mbunge wao jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Singida mjini kwa ajili ya kuhudhuria kampeni za Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dk.John Pombe Magufuli pamoja na kumuombea kura kwa wana Singida.
Pichani juu na chini ni Mohammed Dewji akibadilishana mawazo na watoto waliojitokeza kumpokea uwanjani hapo.
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akiagana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Bumbuli ambaye pia ni mmoja wa wanakamati wa timu ya ushindi ya kampeni za Dkt. Magufuli, January Makamba kabla ya kuelekea kwenye viwanja vya Peoples Singida mjini ulipofanyika mkutano wa kampeni za Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dk.John Pombe Magufuli. Kulia ni Msaidizi wa MO, Duda Jumanne.
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akipata picha ya ukumbusho na wanaSingida wanaoishi karibu na maeneo ya uwanja wa ndege wa Singida mjini.
2 comments:
HUO Muonekano hapo ndi uwanja wa ndege!!! Kweli panatua ndege za aina gani? yaani pamoja na kuweko kwenye uongozi na ukihesabika mtu mwenye fedha nyingi si bora ungelipatengeneza badala ya kutoa kanga na vitenge? Mheshimiwa January je umeoana hapo ni sawa na ahadi zinazotolewa kipindi hiki??
Wewe ulie tu hata hizo kashfa zako haziwezi kusaidia wala kubadilisha nia ya Watanzania kwani wameshaamua. Hapa ni kazi tu na CCM madarakani tena 10/25/2015.
Post a Comment