Saturday, October 24, 2015

NASAHA NA DUA KWA WATANZANIA WAKATI WA UCHAGUZI

Ndugu Watanzania wenzangu.
Temebakisha siku leo tu kabla ya kuandika Historia mpya ya nchi yetu tuipendayo Tanzania.Tunakaribia kumpata Rais mpya atakaetuongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Kipindi ambacho ni muhimu sana Kwetu na kwa vizazi vyetu kutokana na umuhimu wa upande ambao wananchi tunataka nchi ielekee.

Bila shaka wote tunataka mabadiliko.Tunataka maisha bora,Elimu bora,Miundo Mbinu bora,huduma bora za afya na kijamii,ajira pamoja na Serikali yenye kujali raia wake.Hayo yote yanawezekana ikiwa tutaweza kuendelea kuidumisha amani ambayo tumeweza kuilinda kwa miaka zaidi ya Khamsini.

Hii ni hazina kubwa sana kwa nchi yetu ambayo tusithubutu kwa njia yoyote kuivuruga.Ili tuvuke challenge zetu hatuna budi kukumbushana umuhimu wa kuendelea kuitunza amani tuliyonayo Tanzania.Huo ni wajibu wa kila Mtanzania mwenye mapenzi ya Kweli na Taifa letu.Vurugu za aina yoyote zitachangia kudumazika kwa nchi yetu lakini kubwa na hatari zaidi pale zitakapopelekea kumwagika damu ya Mtanzania.

Tuwakemee wachochezi wa aina yoyote ili tuweze kuvuka kwa salama na amani.Wanadiaspora tunawatakia uchaguzi mwema.Maombi na sala zetu tunazielekeza kwenu mlio nyumbani Tanzania.Ameen.

Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu Ibariki Africa.

Hajji Khamis
Mwenyekiti,
Tanzanian Community,
New York,New Jersey,Connecticut na Pennsylvania.

No comments: