Watanzania wenzangu!
Leo tarehe 29 October 2015, kwa kupitia Mgombea Mwenza wangu, Mh. Juma Duni Haji nimewasilisha rasmi malalamiko yetu kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi mkuu wa 2015 kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Tumeainisha kwenye malalamiko yetu, kutokuridhishwa kwetu na mwenendo na matukio mbalimbali, hususani, utangazaji wa matokeo batili, yasiyo akisi matokeo halisi yaliyopatikana kwenye vituo vya kupiga kura, kama ifuatavyo.
• Upunguzwaji wa kura zangu
• Kuongeza kura kwa mgombea wa CCM
•Tunaendelea kukataa dhuluma hii dhidi ya matakwa ya wananchi, na jaribio la kutaka kubakwa kwa Demokrasia kunakooneka wazi kutokana na mwenendo wa Tume kuendelea kutangaza matokeo ya kura yasiyo ya kweli kwa kupoka ushindi wetu.
Aidha, kumekuwepo pia na uporaji wa ushindi kwa wagombea wa vyama vya UKAWA kwenye ngazi ya Ubunge na Udiwani
Kama tulivyoeleza jana takwimu zetu sisi zilionesha kwamba nilikua naongoza kwa zaidi ya 67%,na sasa tumejiridhisha kwamba nimepata kura 10,268,795 sawa na asilimia 62% baada ya kukamilisha kazi ya kukusanya fomu za matokeo nchi nzima.
Kwa hali hii, ninaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi initangaze mara moja mimi EDWARD NGOYAI LOWASSA kuwa mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.
Naendelea kuwashukuru wananchi kwa imani yenu kwangu na kunichagua, MImi, pamoja na viongozi wenzangu tunaamini kuwa kuchezea Demokrasia ni kuvunja Amani, lakini sote tunatambua ni nyie watanzania ndio mnaoporwa haki yenu ya kupata mabadiliko, na viongozi mnao wahitaji, hivyo nitaendelea kuwa pamoja na watanzania wote kudai haki yenu kwa nguvu zote.
Tanzania kwa miaka mingi imefahamika kama kisiwa cha amani katika Afrika, tunashangaa leo kuona vyombo vya ulinzi na usalama vikitanda kila mahali wakiwa na silaha za kivita mitaani kana kwamba uchagzui ni vita, hii ni kuwatisha wananchi ili wakubali kunyang’anywa haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanao wataka, nina amini watanzania hatutakubali hali hiyo.
Lowassa, Edward Ngoyai.
29.10.2015
12 comments:
Usitutishe Wapiga kura, hatukuchagua kwa sababu wewe siyo muadilifu ,mwongo, na mwenye tamaa ya ukubwa ambaye unaweka your personal interest and ego ahead of country. Unawashawishi wapiga kura wafanye fujo? Are you crazy? It won't happen sir, because Tanzania is larger than Lowasa and Sumaye. Why can't you accept defeat graciously?
Unaona? eti lowasa nathubutu kuupotosha umma kwamba angeshinda kwa asilimia 67%? Wewe lowasa hasa licha ya akili yako kutawaliwa na ufisadi kweli unaweza kufikiri unaweza kumshinda magufuli?
Labda huo uchaguzi ufanyike monduli peke yake. Wewe lowasa na wanao kushabikia mtambue kuwa ikiwa jumuia za kimataifa zimethitisha kuwa uchaguzi ulikuwa wa huru na haki basi hakuna mtachokifanya kuyabadilisha matokeo sana kukijengea sifa mbaya chama chenu kuwa ni chama chenye kukataa matakwa ya wengi. Ujinga wenu ni sawa na upuuzi wa kelele za chura bwawani ambazo hazina nguvu yeyote kumzuia mtu wa kuyatumia maji.
mtoa mada usikurupuke hao waangalizi wanachoangalia sio namba ni upigaji kura bila fujo. kama alivyosema mwenyekiti wa tume Mstaafu Jaji, nanukuu "Tunawaruhusu waangalizi wa kimataifa waje kuangalia tunapipiga kura LAKINI HATUTAWARUHUSU KUINGIA JIKONI" mwosho wa nukuu. umeliele2waje hilo! kwani mafisadi ni Lowassa sio basi nakuhakikishia mafisadi wakubwa wako ndani ya Serikali ya CCM na kama unafuatilia anza kufuatilia kuanzia siku anaapishwa na baada ya miezi mitano yote yamesahaulika ufisadi utaendelea huo umeme ulioahidiwa basi utasdissongezeka mgawo na hakuna wale waaagiza sukari wataendelea kuagiza nba kuifanya bidahaa hiyo kuwa ya ghali sana. wahurumie nduguzako wanaotaabika na kutoweza kuwalipia wadogo zako shule!! Yote ni heri tu hakuna wa kushinDANA NA ccm kwani ndio wenye dola! vyama vingi vitafutwa Tanzania siku sio nyingi> amani kwenu.
Lowasa kukatwa ni desturi yake.Hayati baba wa taifa Mwl.Nyerere alimkata, Bunge likamkata kwa ufisadi, CCM wakamkata wakati wa mchakato na sasa wananchi wame mkata...
Hata Savimbi alipinga matokeo.
Acheni ushabiki wenu wa kijinga sisiemu walikuwa wanakusanya matokeo Kituo kwa kituo ikifanya UKAWA human traffickers. ZnZ maalimu aliwawahi na he put them in the box ndiyo maana matokeo yamefutwa. Sikuona Kota lolote la jinai watu kujitolea kukusanya matokeo na kujumlisha. Ndiyo maana Dar majimbo yote yameenda upinzani sasa ya technology kila mtu ana siku na laptop wameshindwa kuchakachuaTanga, Mbeya na Mwanza kura za Lowasa zingingetosha kumlipa magufuli kura zake za vijijini na EL kuibuka mshindi. Sisiemu ndiyo Polisi, Mahakama na Tume upinzani hauwezi kushinda hata siku moja. Kuna haja ya upinzani kujifunza kutokana na hili na kufanya marekebisho makubwa sana kwenye mfumo mzima wa uchaguzi ili uchaguzi uwe huru na haki
WATU WENU FEKI WA IT KUTOKA KENYA,UK NA CHINA WALIOKAMATWA WAMEWADANGANYA SASA MTAENDELEA KUISOMA NAMBA. MZEE NENDA KATIBIWE
Unaware this is your fault. You brought someone with credibility baggage to run for your party. You diveded the party by bringing him un-democratically. You lost trust that you built for years as a credible opposition. Tanzanians are not stupid, they saw what you wanted, it was all about power without any respect for democratic principles. blame yourselves. You chose Lowassa for your party, of all people. Lassus or mnyika even Zitto would have been much better. You lost Ukawa/ Chadema Game over.
Akili za kushikiwa shida. Kuna tofauti kubwa na ya wazi kati ya mtu anaefanya poll tallying na anaefanya poll manipulations. Hiyo IT yenu ya mamluki inajulikana ni nini ilikuwa inafanya na ndio maana viongozi wako walitaharuki kila mmoja akitoa statement yake,na asubuhi na mapema mwenyekiti wako akatia timu mahakamani,changanya akili zako ,sio kutuendelezea sanaa hapa.
Kwa uadilifu wa Lowasa,ulitegemea apambane na ufisadi huo ulio ueleza?
Kwasasa hivi,hayo unayoongea ni maneno ya mkosaji, sisi tuko mbele kwa mbele kujenga taifa letu.
✌✌💗✌✌
Dr Slaa was a credible candidate but we brought a thug and an opportunist as our flag bearer and expected victory? I am proud to be a Tanzania. We choose leaders not gangsters.
Post a Comment