.Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akifurahia jambo na Bi Ikponwosa Ero mwenye Ualibino mara baada ya mazungumzo yao ambapo walibadilisha mawazo kuhusu pamoja na mambo mengine, changamoto zinazowakabili watu wenye ualibino na namna gani jumuiya ya kimatifa inaweza kushirikiana katika kuzikabili changamoto hizo. Bi Ikponwosa aliteuliwa mwezi Agosti Mwaka huu na Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa kama Mtaalamu huru anayeendesha kampeni, uhamasishaji, uelimishaji na uwezeshaji kuhusu watu wenye ualibino na changamoto zinazowakabili watu wenye ualibino. Bi Ero ni Mzaliwa wa Nigeria mwenye uraia wa Canada.
"Mambo poa Balozi, Asante sana," ndivyo anavyosema Bi. Ikponwosa Ero kwa kiswahili fasaha ambacho amejifunza katika safari zake kadhaa nchi Tanzania zilizomfikisha Geita. Bi. Ero amemuahidi Balozi kwamba atasaidia katika kupigia chapuo Azimio lililowasilishwa na Tanzania kwa kushirikiana na Malawi, azimio ambalo linatoa kipaumbele pamoja na mambo mengine, upatikanaji wa huduma za afya, huduma ambayo ni ya muhimu sana kwa watu wenye ualibino kutokana na hali zao hususani matatizo ya ngozi na macho
Kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ualibino, Wakilishi za Kudumu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Malawi katika Umoja wa Matifa, zimewasilisha rasimu ya azimo kuhusu watu wenye ualibino.
Rasimu ya azimio hilo inalenga katika kuzishawishi na kuzitaka Jumuiya ya Kimataifa kuendelea na juhudi za kutetea haki na ustawi watu wenye ualibino ikiwa ni pamoja na kuliwada.
Azimio hilo limewasilishwa kupitia Kamati ya Tatu ya Utamaduni, Haki za Binadamu na Jamii ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, na ambalo limekwisha kusambazwa kwa nchi wanachama na wadau wengine kwaajili ya kupata maoni na kuungwa mkono.
Azimio hilo linajielekeza pia katika kusisitiza upatikanaji wa fursa za elimu, huduma za afya na ajira kwa watu wenye ualibino maeneo ambayo ni changamoto kubwa kwa watu wenye ualibino.
Kupitia azimio hilo, Tanzania na Malawi, zinaitaka Jukumuiya ya Kimataifa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na nchi ambazo tayari zimejiweka sera, sheria na mipango ya, pamoja na mambo mengine, kuwalinda watu wenye ualbino na kuwapatia fursa mbalimbali za maendeleo kama raia wengine.
Vile ile azimio hilo linamwomba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuwasilisha taarifa kuhusu hali za watu wenye ualibino mkazo ukiwa katika changamoto wanazokabiliana nazo, na juhudi ambazo zimechukuliwa na nchi wanachama katika kuzikabiliana nazo.
Taarifa hiyo ya Katibu Mkuu inaombwa kuwasilishwa wakati wa Mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa chini ya ajenda ya Maendeleo ya Jamii.
Azimio hilo pia linasisitiza haja na umuhimu wa kutambua juhudi zinazofanywa katika ngazi ya nchi na Ki- Kanda, na hivyo Katibu Mkuu anaombwa kuwasilisha wakati wa Baraza Kuu la 71 la Umoja wa Mataifa, mapendekezo ya namna ya kuimirisha uwezo na juhudi za nchi husika katika kulitafutia ufumbuzi tatizo la watu wenye ualibino kwa kadri nchi hizo zitakavyoomba.
Katika sehemu ya utangulizi wa Azimio , Azimio linatambua juhudi mbalimbali na taarifa za vyombo vingine kama Vile Baraza la Haki za Binadamu, Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu haki za watu , kuzuia vitendo viovu na ubaguzi dhidi ya watu wenye ualbino pamoja.Azimko linaeleza hofu dhidi ya uovu wanaofanyiwa watu wenye ualibino wakiwamo wanawake na watoto.
No comments:
Post a Comment