Advertisements

Wednesday, October 7, 2015

TUME YAWAASA WANANCHI KUTOSIMAMA KATIKA VITUO VYA KUPIGIA KURA

Na Anitha Jonas- Maelezo
7/10/2015
Dar es salaam
Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini amewaasa wananchi kutosimama katika vituo vya kupiga kura mara baada ya kupiga kura oktoba 25 mwaka huu kwani mawakala wa vyama vya siasa wa kuwepo katika vituo vya kupigia kura ili kulinda maslahi ya chama pamoja na wagombea wao.

Wito huo umetolewa na  Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva alipokuwa akifungua mkutano wa tume  na waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi na makamanda wa polisi nchini.

Jaji Lubuva amesema kuwa wajibu wa mawakala ni kuangalia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na Tume zinazingatiwa katika mchakato mzima wa kupiga kura, kuhesabu kura na kutangaza matokeo na pia kulinda maslahi ya chama au wagombea wao.
“Changamoto zilizojitokeza katika chaguzi zilizopita ni pamoja na kuwapo na makundi ya vijana wanaohisiwa kuwa ni wafuasi wa vyama vya siasa kuwatisha wapiga kura hasa wakinamama ili wasiende kupiga kura”

“Ni rai yangu kwenu kuhakikisha hilo halijitokezi katika uchaguzi huu kwani kupiga kura ni haki ya kikatiba ya kila mtanzania hivyo tusiruhusu vikundi vya watu kuwa  karibu na eneo la upigaji kura kwa kisingizio cha kulinda kura kwani hii itapelekea uvunjifu wa amani” ameongeza Jaji Lubuva.

Mbali na hayo Jaji Lubuva amesema lengo la kushirikisha Jeshi la polisi kwenye uchaguzi mkuu ni kutambua na kuhakikisha kuwepo kwa hali ya usalama na amani wakati wa uchaguzi kwani uchaguzi huru na wa haki ni lazima uendeshwe katika hali ya utulivu na amani.

Kwa uapande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu amesema kuwa jukumu la jeshi la polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao, kuimarisha ulinzi katika vipindi vyote na haswa kipindi hiki cha uchaguzi, kulinda vifaa vya uchaguzi na kusimamia usalama katika vituo vya kupigia kura.


6 comments:

Anonymous said...

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI.TUNAWAHESHIMUNI SANA NA INAPASWA HILO MULIELEWE SI KWAMBA SISI NI MAZEZETA HATUJUI MNAVYOENDELEA NA NJAMA ZENU CHAFU ZA KIHAINI BAINA YENU NA CCM KUWAPA MWANYA WA KIHALIFU CHAMA DOLA CCM KUIBA KURA ZETU.TUMEGUNDUA NA TUNAZIJUA A MPAKA Z YA NJAMA HIZO CHAFU.SASA,MIMI NIMEPIGA KURA,WEWE TUME UNANIAMBIA NIRUDI NYUMBANI.NIRUDI? KWANI TUNATOKA KWENYE MAZISHI? KISHA IWEJE NANI HAPO KITUONI ANAYEKUJA?ACHENI UJINGA HUO.HIZO NI OLD OBSCURE TACTICS ZA CCM.ITAKUA HIVI,MIMI NITAPIGA KURA YANGU HALAFU MIMI NA WENZANGU TUTAPIGA KAMBI MITA MIA TANO[NUSU KILOMITA]TOKA KITUO CHA KUPIGA KURA PALE TUTAENDESSHA MOBILE SURVELLANCE KUKAGUA NYENENDO ZINAZOTIA SHAKA NA KUKABILIANA NAZO VILIVYO ,NA KISHA BAADA YA UCHAGUZI KURA ZITAHESABIWA SISI KIMYA,MATOKEO YA UCHAGUZI YATABANDIKWA NDIPO TUTAKAPORUDI VITUONI KUYASOMA NA KUANZA SHEREHE ZETU RASMI,HATUZUILIKI,HAZUILIKI MTU HAPO.KISHA TUTASINDIKIZA TUKIYALINDA MATOKEO HAYA HADI JIMBONI HADI BAADAYE NEC MAKAO MAKUU. KWA HAPA DAR-ES-SALAAM KWA UCHACHE TUNAWEZA KUWA WANANCHI MILLION MBILI.RAI YETU YA AWALI KWA POLISI NA VYOMBO VINGINE VYA DOLA.MTULINDE TUU,SISI SIO RAIA WA FUJO,HAPANA,NI WA AMANI.MSIJE MKATUCHOKOZA KWA KUTUMIA NGUVU,AMANI ITATOWEKA KABISA NA TENA NI TANZANIA YOTE.RESTRAIN KATAENI AMRI ANGAMIZI,ISIJE IKAANDIKWA HISTORIA TUSIYOIKUSUDIA NCHINI MWETU,HIFADHI..

Anonymous said...

Hatuelewi nia yako ya kusimama kituoni baada ya kupiga kura ni nini! Kama maajenti wa chama chako watakuwepo kituoni muda wote wewe wasiwasi wako ni nini. Au hata maajenti wenu hao huwaamini? Pamoja na haya yote mtu akisoma ulichoandika inaonyesha kuwa wewe siyo muungwana na una ajenda ya vurugu kwani ungekuwa mstaarabu ungethamini yale wengi wanayataka - kupiga kura na kuondoka sehemu hiyo ili wengine wajisikie huru kwenda na kupiga kura zao.

Anonymous said...

RUDIA TENA MAELEZO YANGU,TENA NA TENA INAELEKEA WEWE NI MJINGA WA ASILI WA KUZALIWA.SOMA MAELEZO YANGU MARA MIA.NIMESEMA BAADA YA KUPIGA KURA MIMI NA WENZANGU TUTAONDOKA VITUONI TUTAPIGA KAMBI NUSU KILOMITA YAANI MITA MIA TANO TOKA VITUONI.UMBALI WA KUTOKA ROUND ABOUT MSIMBAZI HADI KARUME.JEE BADO TUPO KITUONI AU HUVIJUI VIPIMO.ULITAKAJE MSIMBAZI HADI BUGURUNI?SASA TUKIWA KARUME TUTAMFANYA NANI ASIJISIKIE KWENDA KUPIGA KURA,MKEO?ACHENI UPUMBAVU WENU.MWAKA HUU ITAKUA TOFAUTI KABISA NA MIAKA YOTE YA UCHAGUZI,TUMEHAMASIKA.KWAKO TENA WEWE ULIYETUMWA.UCHAGUZI HUU UTAKUA NI WA UTULIVU MKUBWA NA AMANI TELE.SISI TUTAJITOKEZA KWA MAMILLION KUMCHAGUA KIPENZI WETU MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA NA TIMU YAKE YA WABUNGE NA MADIWANI.TUKISHA WACHAGUA,TUTALINDA KURA ZETU KIINTELIJENSIA[HUMO TUMO TULIOENDA SHULE SANA TENA SANA] TUTASUBIRI-KITUO KWA KITUO- KURA ZIHESABIWE,MATOKEO YABANDIKWE,TUTAYASOMA KITAKUA KIMEELEWEKA,NA BAADA YA HAPO,MAMA YANGU WEEEEE KITIMTIM,TUTAANZA KUUSHANGILIA USHINDI WETU KIAINA AINA,AS NEVER SEEN BEFORE.HILI HALINA MJADALA,USHINDI WETU NI WA UKOMBOZI WA PILI.KALAGABAHO WE KISOKOROMBINGO MGONA HOVYO.

Anonymous said...

Kuendelea kubishana, watu hawawezi kuona tofauti!

Anonymous said...

A CCM COMMITED FOOL WILL NEVER BE EDUCATED.HE OR SHE WILL ALWAYS KEEP URGUING NON-SENSELY.KEEP YOUR LOCKS TIGHT.

Anonymous said...

Don't argue with a fool as people will notice the difference!