Sunday, October 25, 2015

Uchaguzi wahairishwa kwa kukosa karatasi za udiwani

By Faustine Fabian, Mwananchi
Bariadi. Wakati zoezi la upigaji kura likiendelea nchi nzima wakazi wa kata ya Matongo, jimbo la Bariadi, mkoani Simiyu wameshindwa kupiga kura kwa nafasi ya udiwani kwa kile kinachodaiwa uhaba wa karatasi za kupigia kura.

Akiongea na waandishi wa habari Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo Abdallah Malela amesema kukosekana kwa karatasi ndicho chanzo cha uchaguzi kwa ngazi ya udiwani kusitishwa katika eneo hilo.

Alisema kuwa kata hiyo ina jumla ya wapiga kura 7500, na vituo 17 lakini karatasi ambazo zimetoka Tume ya ucHaguzi zilikuwa 3400 tu, huku zaidi ya wapigakura 4100 wakikosa karatasi hizo za kupigia kura.

“Baada ya kuona hali hiyo niliwasiliana na viongozi wa tume kutoa taarifa ambao waliamua kuhairisha zoezi kwa nafasi ya udiwani tu, mpaka tena itakapotangazwa na tume,” alsiema Malela.

Kwa upande wa rais na mbunge, zoezi liliendelea kama kawaida kwa kuwa karatasi hizo zililetwa za kutosha.

Kwa upande wa Jimbo la Itilima Mkoani hapa Msimamizi wa uchaguzi Alphonce Aloyce alisema zoezi lilienda salama licha ya mihuri kukwama ingawa tatizo hilo lilipatiwa ufumbuzi mapema.


7 comments:

Anonymous said...

Nchi hii uzandiki tu. Ipo siku tutaamka tu.

Anonymous said...

Tatizo tume wamewapa majangili yao, za kuchakachulia ndio maana kuna upungufu

Anonymous said...

Huu ni ujinga usio eleweka sasa

Anonymous said...

Mmh priorities magumashi too much talking aarg

Anonymous said...

Wacha uzandiki wako. Hata nchi nyingine matatizo madogo madogo kama haya hutokea. Wewe kaa chonjo na ulie tu maanake leo ni mwisho wa Chadema na Ukawa yenu. Mtakipata.

Anonymous said...

I swear Tanzania itaendelea kuwa Tanzania tuuu,am not even surprise anymore

Anonymous said...

Sawa kabisa, Tanzania itaendelea kubaki Tanzania. Ulifikiria siku moja itakuwa Marekani? Wengine tunaridhika na Utanzania wetu na nchi yetu. #Hapa kazi tu!!!!!!!