Advertisements

Sunday, October 18, 2015

WATOTO BADO WANAENDELEA KUDHULUMIWA UTOTO WAO- UMOJA WA MATAIFA

picha hii kutoka maktaba inamwonyesha mtoto ambaye anatumika kama askari na hivyo kumnyima haki yake ya msingi ya kuishi utoto wake, pamoja na kupata huduma zake za msingi kama vile afya, elimu, malenzi na ukuaji wenye hadhi. Pamoja na Umoja wa Mataifa kuendelea na kampeni yake ya kupinga watoto kutumika kama askari, bado taarifa za hivi karibu za Umoja wa Mataifa, zinaeleza kuwa watoto bado wanaendelea kutumika katika baadhi ya maeneo kama askari, huku wengine wakiingizwa katika biashara haramu zikiwamo za ngono.
Bi Vickness Mayao kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, akichangia majadiliano kuhusu haki za mtoto wakati wa Mkutano wa Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Kamati iliyokuwa ikijadili kuhusu haki za mtoto ambapo akizungumza kwa Niaba ya Serikali Bi. Mayao amesema Serikali inaendelea na uboreshwaji wa Sheria mbalimbali zinazolinda haki ya Mtoto huku ikisisitiza kwamba wajibu wa kwanza wa kumlinda mtoto dhidi ya madhara yoyote ni ya Wazazi wenyewe. aliyekaa nyuma ni Afisa mwingine kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Grace Mbwilo
Pamoja na kufanyika kwa mikutano ya Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Mikutano ya Kamati nyingine zikiwamo ya Pili inayohusika na masuala ya Uchumi na Maendeleo pia imekuwa ikiendelea na vikao vyake. Pichani ni Bw. Ahmed Makame Haji Kamishna wa Tume ya Mipango kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwa katika moja wa Mikutano ya Kamati ya Uchumi na Maendeleo wapo pia Bi. Halima Wagao kutoka Wizara ya Fedha ( ZNZ na Bi. Mtumwa Idrissa kutoka Tume ya Mipango ( ZNZ)
Bw. Suleiman Said Ali. Afisa Mambo ya Nje , Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ( ZNZ) akifuatilia Majadiliano ya Kamati ya Nne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, iliyokuwa ikijadili kuhusu masuala ya misaada ya ulipuaji wa mabomu ya Ardhini, Bw. Ali pia alishiriki katika Majadiliano ya Umalizwaji wa Ukoloni kwa Makoloni 17 ambayo bado hayajapata fursa ya kujitawala na kujiamulia mambo yake yenyenyewe likiwamo Koloni la Western Sahara, koloni pekee barani Afrika.

No comments: