Wiki kadhaa nyuma mfanyabiashara mkubwa na maarufu Tanzania Mohamed Dewjialiweka wazi dhamira yake ya kutaka kuinunua klabu ya Simba na kuwekeza bilioni 20 kwa ajili ya klabu hiyo, Dewji lengo lake ni kununua hisa asilimia 51 za klabu ya Simba na kuiwezesha ifike mbali.
Taarifa za Dewji kutaka kuinunua klabu hiyo zilitoka wiki kadhaa nyuma na kuthibitisha kuwa tayari ameeleza dhamira ya lengo lake hilo kwa Rais wa sasa wa klabu ya SimbaEvans Aveva na kumwambia aandike barua rasmi ya kuomba kuuziwa klabu hiyo, Stori za November 4 mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo Ismail Aden Rage ameeleza mtazamo wake kuhusu wazo la Mohamed Dewji, vipi kama angekuwa yeye ndio Rais angefanyaje?
Ismail Aden Rage
“Tatizo ni kwamba wanachama wetu sisi wanapenda tu vilabu vyao na mashabiki wanapenda kuchangia michango yao kwa kulipa viingilio uwanjani ila tatizo ni kwamba vilabu vyetu havipati udhamini wa maana ila usidhani kama mtu mmoja pekee anaweza kufanya mabadiliko katika mpira hakuna duniani mafanikio kama hayo”>>> Aden Rage
“Kama ningekuwa Rais wa Simba kwa sasa kuhusu suala la mtu kumiliki hisa nyingi katika klabu kwanza ningefanya utafiti wa kuangalia Hispania wanafanya nini, Ujerumani wanafanya namna gani,baada ya hapo ningelipeleka kwa wanachama kwa sababu ile klabu sio ya kwangu”>>> Aden Rage:Credit:MillardAyo



3 comments:
Hao akina Rage ndio wanaonufaika na hali ya simba ya sasa kwanini amepewa nafasi ya kutoa mawazo yake? Huyu Aden Rage hafai hata kuchangia juu muustakabali wa simba kwani yeye ni miongoni mwa wanaozorotesha maendeleo ya simba. Kwanini tuende Hispania au Ujerumani tusiende kwa Katumbi au Baharesa? Na kwa simba ya sasa haina haja yakwenda hata kwa katumbi jinsi ya kujifunza vipi klabu inaendeshwa bali watakiwa kujifunza kutoka Stand United ya Shinyanga. Kocha yule mfaransa walisema hafai sasa anawasuta. Mtoto yule mdogo kabisa lakini mungu kamjalia maungo yaliyoshiba aina ya wachezaji Tanzania siku zote inalia kuwa wamepotea katika miaka ya hivi karibuni sasa bahati iliwadondokea simba kuwa na aina ya mchezaji huyo wangemlea na kumtunza vizuri hakika simba ingenufaika muda si mrefu wangekuwa na uwezo wa kumuuza nje kwa maslahi mazuri zaidi kuliko ya samata au Okwi hapa nazungumzia Eliasi Maguri. Kwa kweli huyu kijana ni hazina ya Taifa katika mchezo wa soka ningeomba wadau wenye uweledi wa soka huko nyumbani wae karibu nae ili kumpa ushauri wa maana ili kutunza kipaji chake kwani ukijumlisha na umbile lake na umri wake hakika maguri ni aina ya wachezaji wenye solo kubwa sana ulaya. Nashangaa simba kumuachia bure bure? Kwa hivyo kwa manufa na maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania na simba kwa ujumla bila ya ubishi wowote Mo anapaswa kupewa nafasi ya kuinunua Simba tena ikiwezekana haraka tu. Kwanza ningeomba kuchukua nafasi hii kumpongeza Mo kwa nia yake hiyo na uzalendo aliounyesha. Tunaimani viongozi wa simba kwa kushirikiana na wananchi hawata iachia fursa hiyo muhimu kwa maendeleo ya klabu ipotee hivi hivi na kuendelea kudumisha ubabaishaji klabuni hapo.
Simba oyee, msimbazi kwanza.
Anzisha team yako kama Azam alivyofanya.Hizi team kubwa za Simba na Yanga iko siasa mingi watakuzengua in a long run.
NILIVYOMUONA RAGE TUU,NIKASHUSHA PUMZI.SI YEYE KATUMWA.RAGE NI TAPELI, MWIZI,MUONGO,MFIINISHI. KAJINUFAISHA SANA AKIWA SIMBA,KAUPATIA UBUNGE SIMBA.KWA UJUMLA NI MWIZI NA NDIYO MAANA AKIWA KATIBU MKUU FAT YA NDOLANGA ALIIIBIA FAT ILE NA AKAFUNGWA.
Post a Comment