Kufuatia agizo la Rais John Magufuli alilotoa hivi karibuni la kusitisha safari za nje kwa wizara, idara na taasisi za serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeanza kutekeleza kwa kutoa maelekezo kwa Balozi zake za nje.
Wizara hiyo imezielekeza Balozi zote zilizopo maeneo mbalimbali duniani kujipanga ili kushiriki kikamilifu katika kuiwakilisha serikali kwenye mikutano yote ya kimataifa na kikanda inayofanyika katika maeneo yao ya uwakilishi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam na wizara hiyo, imeeleza
Tanzania ina Balozi 35 zikiwamo bazozi ndogo tatu, vituo viwili vya biashara na konseli za heshima 17 katika nchi mbalimbali.
“Hizi zote zitahusika katika kuendeleza utekelezaji wa diplomasia yetu ya uchumi na uwakilishi wa maslahi ya nchi yetu,” ilieleza taarifa hiyo.
Hadi sasa mikutano ambayo tayari imefanyika na Balozi zetu kuwakilisha ni pamoja na Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoendelea nchini Malta na Mkutano wa Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Habari wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika nchini Lesotho.
Aidha, imetoa wito kwa wizara, idara na taasisi za serikali kuwasilisha mapema taarifa za mikutano inayohusu sekta zao ili kutoa fursa ya kuzianyia kazi kwa wakati na kuhakikisha ushiriki wa Tanzania unakuwa wenye tija kwa taifa.
Ilieleza kuwa wizara inaungana na wadau wengine kumpongeza Rais Magufuli kwa hatua anazozichukua za kuleta ufanisi mkubwa wakazi na kubana matumizi ili kuiwezesha serikali kuwahudumia wananchi.
4 comments:
Mheshimiwa Raisi wakati umefika wa kusafisha balozi zetu.Ondoa watumishi wasiokuwa na sifa weka watu makini watakaokuwa na uwezo wa kutekeleza mission hii.Tuache kuchaguwa mabalozi na watumishi wa balozi zetu kwa vigezo vingine zaidi ya qualifications na uwezo wao.
Nakuunga mkono mdau wa 1:07 AM. Ni muhimu pia kupunguza payroll kwenye balozi zetu. Nyingi ya balozi zetu zinaajiri wafanyakazi wengi ambao hawanufaishi Taifa letu. Mfano mkubwa, balozi zetu pale London-UK na Washington, DC-USA zimewaajiri non-diplomatic personnel wengi ambao siyo muhimu by all measures, na hivyo wanakuwa mzigo mkubwa kwa walipa kodi Tanzania. Mtukufu Rais, tunakuomba uanze kuzisafisha balozi zetu zote. Ni muhimu ukianza kusafisha Wizara ya Mambo ya Nje hapo Dar, kwani ndiyo chanzo cha matatizo.
muheshimiwa mgufuli ili tusiwe na mfumo mbovu endelevu na wasikurudishe nyuma, kama alivyosema mdau hapo juu, qualification ndio inayohitajika si fadhila, ondoa wafadhiliwa wote kwa faida ya taifa, watanzania walioko nje waone faida ya balozi zao na kuwa karibu nazo, sio kuona balozi kama kito cha polisi
Wewe hapo juu Asante umenena.
Post a Comment