Exim Bank ya Tanzania siku ya Jumamosi ilifanya usaili kwa Diaspora Watanzania wanaoishi nchini Marekani jijini New York kwa ajili ya kuwapa kipaumbele Diaspora na hatimaye kuwapatia kazi kwenye Benki hiyo yenye makao makuu yake Dar es Salaam, Tanzania.
Akiongea na Vijimambo/Kwanza Production mkuu wa human resources Bwn. Fredirick Kanga alisema sababu kubwa ya Benki hiyo kuwafanyia usaili Diaspora ni kutambua mchango wao na mfumo wa uchapa kazi waliouzoea ili waweze kuutumia nyumbani katika kuleta maendeleo yenye ufanisi katika sekta mbalimbali kwenye Benki hiyo ambayo kazi kubwa ni kutoa huduma bora kwa wateja wake.
Bwn. Fredirick Kanga akijibu swali ni kwanini wasitafute wafanyakazi waliopo Tanzania ambao wengi wao wamemaliza masomo ya juu na hawana kazi. Bwn. Kanga alisema sababu kubwa ya kuja Diaspora nikutokana na kutambua mchango mkubwa wa Diaspora na ufanisi wao katika kazi na sio kweli kwamba hatuajili Watanzania waliopo nyumbani, tunachojaribu ni kuchanganya ujuzi wa Diaspora na nyumbani ili kufanikisha na hatimae kutoa huduma bora na zenye ufanisi mkubwa, huku akisema Benki ya Exam ndio Benki yenye asilimia ndogo ya makato kwenye akaunti za wateja wao nchini Tanzania.
Bwn. Kanga alisema tangia tuanze kuasaili Diaspora tumeisha wapatia kazi wapatao 25 na mwaka jana pekee tuliwapatia nafasi Diapora 6 toka Uingereza na 3 kutoka nchini Marekani. Baadhi ya Diaspora wanapenda kurudi nyumbani lakini wanahofia jinsi gani ya kuanza maisha yao mapya baada ya kukaa ughaibuni kwa muda mrefu. Exam Benki imeliangalia hilo na ndio sababu kubwa inayowafanya kufanya usaili kwa WanaDiaspora anaporudi nyumbani anauhakika na kazi yake.
Kulia ni Paul Rupia kutoka Massachusetts akifanyiwa usaili na Bwn. Frederick Kanga na Dinesh Arora (kushoto) ambaye ni Chief Executive Officer wa Exim Bank siku ya Jumamosi Novemba 7, 2015 katika hotel ya Hilton katikati ya jiji la New York
Kulia ni Ability Kakama kutoka New York akifanyiwa usaili na Bwn. Frederick Kanga na Dinesh Arora (kushoto) ambaye ni Chief Executive Officer wa Exim Bank siku ya Jumamosi Novemba 7, 2015 katika hotel ya Hilton katikati ya jiji la New York
Kulia ni Pamela Mgema kutoka Texas akifanyiwa usaili na Bwn. Frederick Kanga na Dinesh Arora (kushoto) ambaye ni Chief Executive Officer wa Exim Bank siku ya Jumamosi Novemba 7, 2015 katika hotel ya Hilton katikati ya jiji la New York
Kulia ni Peter Mgema kutoka Texas akifanyiwa usaili na Bwn. Frederick Kanga na Dinesh Arora (kushoto) ambaye ni Chief Executive Officer wa Exim Bank siku ya Jumamosi Novemba 7, 2015 katika hotel ya Hilton katikati ya jiji la New York
Kulia ni Mariam kutoka Columbus, Ohio akifanyiwa usaili na Bwn. Frederick Kanga na Dinesh Arora (kushoto) ambaye ni Chief Executive Officer wa Exim Bank siku ya Jumamosi Novemba 7, 2015 katika hotel ya Hilton katikati ya jiji la New York
Kie Mlay (kulia) kutoka Maryland akiongea jambo na Bwn, Frederick Kanga wakati wa usaili wa kujaribu kuwaoatia Diapora nafasi za kazi kwenye Benki ya Exim yenye makao makuu yake jijini Da es Salaam siku ya Jumamosi Novemba 7, 2015 katika hotel ya Hilton katikati ya jiji la New York..
2 comments:
Hivi Exim bank wamekosa watu back home mpaka kuja ny kutafuta watu kuajiri? Kuna wanafunzi chungu mzima wanamaliza vyuo hawana kazi miaka. Watu wa nyumbani inabidi kupewa kipao mbele zaidi kwenye hizo ajira. USA is the land of opportunity hao jamaa wanatakiwa kutafuta kazi kwenye mabank ya hapa Kama wamesoma sioni ugumu wa wao kupata kazi USA.
HUYU JAMAA HAPO JUU HANA UFAHAMU KABISA. TAMBUA AMERICAN DREAM KWAKO YAWEZA KUWA NIGHTMARE KWA WENGINE. PIA, KUNA TATIZO GANI KAMA IWAPO BENKI KAMA EXIM INATAFUTA WATU WENYE FIKRA TOFAUTI NA WALIOKO BONGO. JIFUNZE KUFIKIRI NJE YA BOKSI NA UWE MZALENDO KATIKA KUUNGA MKONO UJENZI WA NCHI YAKO. HONGERA EXIM BANK KWA MFANO ULIO SAHIHI KWA WAAJIRI WNGINE WALIOKO BONGO NA AFRIKA KWA UJUMLA.
Post a Comment