ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 16, 2015

HAWA NDIO WACHIMBAJI WALIOFUKIWA NA KIFUSI KWA SIKU 41.


Watu watano kati ya sita waliofukiwa katika machimbo ya Nyngalata, Kahama kwa siku 41 wameokolewa usiku wa kuamkia leo wakiwa hai.
Watu hao walikuwa wakiishi kwa kula nyura wakiwemo mende na kunywa maji yaliyochanganyika na mikojo Watu hawa  walikuwa umbali wa zaidi ya kilometa 10 ardhini baada ya kuangukiwa na kifusi..
Hivi sasa wamelazwa katika hospitali ya Kahama.



6 comments:

Anonymous said...

asante na tunawapa pole. mbloger, ni vyema tu mkatupa habari bila ya hizi picha za kutisha!! Duuh wanachimba dawa au madini ya aina gani afya ziwe hivyo. !!

Anonymous said...

Mdau, na wewe uwe unasoma ndipo unatoa comment.Hao wamekaa ndani ya shimi chini umbali wa mita 100 kwa siku 41.Walikuwa wanakula magome ya miti, na maji wanayokinga kwa Helmet, ndiyo maana wamedhoofu hivyo.Ila,kwa uhakika hawa watu ni majasiliri.Mungu mkubwa,wameokolewa.

Anonymous said...

Hiyo ndiyo Tanzania ambayo Chama Tawala CCM inajivunia kuijenga miaka zaidi ya 50 baada ya kupata uhuru. Hata kama hutaki kuziona hizo picha lakini ukweli unabaki pale pale, kuna ndugu na jamaa zako wengi ambao wako katika hali hiyo na pngine mbaya zaidi. Kwenye machimbo ya watu binafsi vijana wanafanyishwa kazi kama punda, hakuna vifaa vya kujikinga na hatarishi za maisha yao. Inabidi kufanya kazi kama watumwa, kwa vile tu hakuna jinsi ya kupata riziki nzuri ya maisha.
Miili ya watu inakwisha na kunyong'onyea kama wana utapia mlo.

Hapa ni kazi tuuuuuuuuuuuuu!!!

Anonymous said...

Hivyo watanzania lini tutaacha siasa za kipumbavu hata katika masuala ya msingi. Ajali za migodi watu kuangukiwa na kufukiwa na udongo wakati wakiendelea na shughuli za uchimbaji wa madini hutokea duniani kote hao jamaa kukaa muda wote huo chini ya ardhi zaidi mita mia moja kwa siku 41 na kuwa wazima kwa kweli ni kazi ya mungu kwamba siku zao za kuishi bado zipo.

Anonymous said...

Nimesikiliza maelezo ya Kamanda wa Polisi wa eneo hilo .... Eti wachimbaji hao wanaitwa "manyani" !!!!!

Anonymous said...

Inasikitisha kuona hata majanga yasiyozuilika yanapotokea tunalalama na kusahau yakuwa kuna ajali kazini katika maeneo mbali mbali ya kazi ajali yaweza tokea. Chile wachimbaji wao walikaa chini siku 30 au 31, walipotoka watu walishukuru na kufurahi na inatarajia kutoka movie ya hao wahanga. Lakini inapokuja kwa Tanzania, tunabakia kulaumu tu ndo maana hata maendeleo hatupati kwa sababu hakuna cha kushukuru! Mafuriko yakitokea Tanzania, utawasikia wakilalamikia serikali lakini yakitokea marekani au australi tena makubwa, hatuwasikii. Tubadirike na tumshukuru Bwana hao watu wameokolewa na family zao zina furaha kwa hilo japokuwa wewe unaona wanakuabisha!