ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 16, 2015

MAYUNGA NALIMI KUJA MAREKANI KUREKODI VIDEO NA AKON

Mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi akiongea na waandishi (hawapo pichani) wakati wa tukio la kumuaga kwa ajili ya kuja nchini Marekani. Hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika katika Makao Makuu ya Ofisi ya Airtel Morocco jijini Dar Es Salaam. Pichani katikati ni Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde, akifatiwa na Mwalimu wa sauti Tony Joet.
Ofisa Uhusiano na Mwandamizi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Aristed Kwizera (kushoto) akimuaga mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi. Anayeshuhudia (katikati), ni Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde.

MSHINDI wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga ameondoka nchini Tanzania jana kuja Marekani kwa lengo la kupata mafunzo na kurekodi nyimbo yake. Nalimi Mayunga ameondoka jana usiku, kwenda kufanya kazi na nguli wa mzuki wa R&B nchini Marekani, Akon ambapo anatarajiwa kukaa huko kwa muda wa wiki moja kisha kurejea nyumbani Novemba 24, mwaka huu.

Akiongea wakati halfa ya kumuaga, Ofisa Habari Mwandamizi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Aristide Kwizera alisema” Tunajisikia furaha kuona vijana wa kitanzania wakitangaza sanaa na nchi yetu duaniani kupitia muziki. Napenda kumpongeza sana mayunga kwa kupata ushindi ambao umempatia nafasi hii nono na kumwomba atumie vyema fursa hii. Sisi kama wadau wakuu wa sanaa nchini tunawapongeza sana Airtel kwa kuanzisha program zenye lengo la kukuza sanaa na muziki wa nchini kama hii ya Airtel Trace Music Stars na nyingine nyingi.

Naye mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga alisema” ile siku niliyokuwa naisibiria kwa hama leo imefika na nimejipanga kuondoka kwenda kujifunza mengi na ya msingi katika maisha yangu ya muziki . Naamii safari hii itakuwa ni ya mafanikio makubwa na mwanzo wa hatua yangu ya mafanikia katika tasinia ya muziki

Napenda kuwaambia watanzania wajiandae kusikia kibao na video kali ntakayoifanya na Akon kwani nimejiandaa vya kutosha kuhakikisha nashirikiana nae vyema ili tunatoa nyimbo kali itakayowapa burdani wapenzi wa muziki pande zote duniani. Aliongeza Mayunga

Kwa upande wake Aliyekuwa jaji katika shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania na Mwalimu wa Muziki Tony Joet alisema” mayunga amekuwa akifanya mazoezi kujiandaa kwa deli hii toka alipotangazwa mshindi wa Airtel Trace Afrika. Ninaimani naye kwani ameonyesha uwezo mkubwa na nidhamu ya hali ya juu na naamini atafika mbali na namtakia kila laheri katika safari yake”

Akiongea kwa niaba ya Airtel Ofisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema” mipango yote ya safari imekamilika na mayunga atakuwa marekani kwa muda wa wiki moja, tunaamini mayunga atakaporejea atakuwa tofauti kabisa na alivyokwenda na ndio hasa lengo letu sisi Airtel, kuwawezesha

No comments: