ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 29, 2015

Hospitali za Apollo Kutoa Huduma za Kiafya Saa 24 kila siku Ulimwenguni Kote

Bi. Sangita Reddy, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali za Apollo

Na Mwandishi Wetu ,

Kurahisisha huduma za afya ulimwengu kote, watojia wakubwa wa huduma za afya kundi la hospitali za Apollo limebuni njia mpya madhubuti ya utoaji wa huduma za afya inayoitwa; Ask Apollo, njia bora mpya mahususi kwa wagonjwa walio mbali. Hii inathibitisha kupiga hatua zaidi kwa hospitali za Apollo na katika uwanja wa afya ulimwenguni.

Jitihada hizi kutoka hospitali za Apollo zitajenga mahusiano rahisi ya mgonjwa-huduma zitakazo mpa mgonjwa mbadala wa kuwasiliana na daktari mahali popote na muda wowote watakao kubaliana. Kupitia Ask Apollo, mgonjwa anaweza kuweka miadi na daktari wa mambo ya familia,mlo kamili na mambo ya afya, ushauri kutoka kwa wataalam au bodi ya wataalam kutokana na uhalisia wa tatizo.

Akitoa maoni katika ufunguzi, Ms. Sangita Reddy, mkurugenzi mtendaji wa hospitali za Apollo alisema “kupitia Ask Apollo, tunaendeleza kundi la Apollo litakaloacha urithi mkubwa kwenye kutengeneza mandhari na kuchangia kuinua viwango vya utoaji huduma za afya. Hospitali za Apollo zina nia ya kuleta mapinduzi kupitia teknolojia kupitia program ya Ask Apollob ambapo mgonjwa anaweza hadi kuchagua daktari anayempenda na kupanga muda atakao hitaji kuonana nae. Ask Apollo ni 100% huduma ya kimtandao hivyo inaondoa uhangaikaji wa kusafir kwenda kliniki au hospitali na kukaa kwenye foleni ndefu.”

Kujifunza mengi kuhusu “Ask Apollo”, mtumiaji anaweza kuingia kwa www.askapollo.com na kupata huduma za Ask Apollo, aliongeza Mkg. Sangita Reddy.

Watanzania wanashauriwa kufaidika na huduma za kiafya kutoka Ask Apollo pindi wanahitaji huduma bora za kiafya kwa magonjwa makubwa au sugu. Ask Apollo ni huduma yenye gharama nafuu lakini pia inawafaidisha wagonjwa waliopo mbali. Wagonjwa kutoka Tanzania wanaweza kupata huduma hii kutoka kwa wataalam muda wote masaa 24 kwa wiki kutokana na ukubwa wa tatizo. Huduma hii ya kimtandao inaokoa muda, pesa, na usumbufu wa watanzania kusafiri mara kwa mara kwa ajili ya huduma za afya hospitali za Apollo.

Hospitali za Apollo zimechukua hatua madhubuti kwenye kuboresha huduma za afya. Umakini katika zoezi hili umeongeza kasi kwenye kupata taarifa na muda wa kuzipata katu ya mgonjwa na daktari. Nia hii ya hospitali za Apollo ni hatua katika kuboresha upatikanaji bora wa huduma za afya ulimwenguni.

Huduma ya Ask Apollo inalenga mambo makuu yafuatayo; mfumo wa upumuaji na moyo (Cardiology), afya ya uzazi wa mama (Gynecology), mfumo wa fahamu na ubongo (Neuro Surgery), mfumo wa mkojo (Urology), daktari wa watoto (Pediatrician),maumivu ya miguu na viungo (Rheumatology), matatizo ya ngozi (Dermatology), matatizo ya akili (Psychiatry), matatizo ya nevu (Nephrology), upasuaji wa uvimbe (Surgical Oncology), miale kwa ajili ya kuondoa uvimbe (Radiation Oncology), matibabu ya uvimbe (Medical Oncology), madawa ya ndani na upasuaji wa uvimbe katika kichwa na shingo.

Kupitia uwanja huu wa huduma za kiafya, mtu anaweza kuchagua daktari anayemtaka au mtaalam kutokana na aina ya ugonjwa ulio nao, unaweka taarifa zako na kuonana na daktari, program hii itasaidia mgonjwa kupata aina gani za dawa atumie.

Kwa miongo iliyopita, ulimwengu wa afya umekumbana na mabadiliko makubwa ya maendeleo ya kiteknolojia na pia ubunifu uliopelekea mapinduzi katika kumpata daktari na matibabu kwa wagonjwa. Mapinduzi haya kwenye maeneo tofauti ya afya yamesaidia kuimarisha huduma za afya na kuleta matokeo mazuri kwa wagonjwa.

Ongezeko kubwa la utoaji huduma bora za afya na upanukaji wa matumizi yake umechangia sio tu kwenye kuwakutanisha madaktari katika fani zao bali pia kutengeneza uwanja mzuri wa daktari kukutanishwa na wagonjwa.

Kuhusu Hospitali za Apollo

Hospitali ya Apollo ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo "Dhamira yetu ni kuleta huduma ya kisasa karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa huduma bora na mafanikio katika elimu na utafiti kwa ajili ya jamii ya kibinadamu".Katika miaka 30 tokea kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo imeandika historia kubwa kupata kuonekana nchini India. Ni moja ya kampuni kubwa ya Afya katika bara la Asia, na pia imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini india.

Katika safari yake, imeweza kuboresha maisha ya watu wapatao milioni 39 kutoka nchi 120.Inatoa huduma maalum 52 na vitanda vya upasuaji 710.Imefanya upasuaji wa moyo wenye kufikia idadi ya watu 152,000 na panuzi 125, 000 za mishipa myembamba.Imefanya upasuaji wa wa viungo unaopita kiasi cha idadi ya watu 10,000, upasuaji wa uvimbe wa ubongo, uti wa mgongo na zaidi.Taasisi ya Apollo ni moja ya taasisi zinazoongoza nchini india, zikiwa na teknolojia za kisasa kama Novalis TX, PET MRI na Upasuaji unaotumia mashine za kiroboti.

8 comments:

Anonymous said...

Muda umefika sasa tuimarishe huduma katika hospitali zetu,hii biashara ya Apollo iwe history.Walichochuma so far kinatosha.

childspecialistnoida said...

www.drnalinagarwal.com
"Address- Ayushman Medicare,
D 83, Sector 26, Behind Nithari Police Chowki, Noida 201301, Uttar Pradesh, India"

Best Child Specialist in Noida
Best Pediatrician in Noida
child doctor near me

websitemaker said...

marketing wise is the best website agency for doctors in Noida .it is web designing company in noida and website designing company in noida also.if you are searching for top web designing companies in noida and web development comapny in noida or web design agency then click on https://www.marketingwise.in

Dr Sandeep jha - Liver Specialist Delhi said...

dr sandeep jha is the Best doctor for liver in delhi .He is the Best Gastroenterologist in Delhi.if you want to meet Live Specialist in Delhi than click here https://www.drsandeepjha.com/

Dr Sandeep jha - Liver Specialist Delhi said...

Dr Sandeep Jha - Best Gastroenterologist in Delhi, Best Liver Doctor in Delhi
dr sandeep jha is the Best doctor for liver in delhi .He is the Best Gastroenterologist in Delhi.if you want to meet Live Specialist in Delhi than click here https://www.drsandeepjha.com/

dr abhishek mishra said...

Dr sudhir kumar is best general surgeon in noida .he is the piles doctor in noida and best hernia surgeon in noida.he is best doctor for anal fistula treatment in noida .if you are searching for anal fissure treatment in noida then click on https://www.drsudhirkumar.in

dr abhishek mishra said...

Dr sudhir kumar is best general surgeon in noida .he is the best piles doctor in noida. All type of surgical treatment for piles or hemorrhoids is available. Call now to get treated by an experienced piles doctor in Noida. Stapler hemorrhoidectomy, laser piles treatment and all advanced treatments available. https://www.drsudhirkumar.in/haemorrhoids-surgery/Dr. Sudhir Kumar - Best General Surgeon in Noida, Best Piles Treatment in Noida, Hernia Repair and Laparoscopic Surgeon

childspecialistnoida said...
This comment has been removed by the author.