Advertisements

Sunday, November 29, 2015

THANKSGIVING HOUSTON SATURDAY FAMILY DAY

Mwanamitindo nguli Asya Idarous Khamsini akijiandaa na onesho la vivazi siku ya Jumamosi Novemba 28, 2015 kwenye sherehe za Thanksgiving zinazo sherehekewa na Jumuiya ya Watanzania Houston, Texas.
 Wachezaji wa Stars United kutoka kushoto ni Saad, Kheri, Baloteli, Ny Ebra, Makubeli na Liga wakijadili jambo baada ya mechi yao na wenyeji Houston kuahirishwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyeshamjini humo katika kipindi hiki. Wachezaji hao walipeleka lawama kwa wenyeji Houston kwa kukodisha uwanja wa nyasi huku wakijua kipindi hiki ni cha mvua. Kawaida viwanja vya nyasi hufungwa kwa kuhofia kuharibika, msimu kama huu wa mvua timu nyingi hukodisha uwanja wa nyasi za bandia ambao haijalishi jua au mvua huchezewa tu. Wachezaji wengine wa Stars United waliokuja Houston lakini hawapo kwenye picha ni Gilles, Tifu, Max, Hassan na Rahim ambaye yeye huishi Houston.
 Wadau wa Houston wakiwa kwenye siku ya familia
 Siku ya familia ambayo ilifanyika mchana Jumamosi Novemba 28, 2015 ikihudhuria na wazazi na watoto wao.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

 Mama na mwana wakiwa katika picha ya pamoja.




No comments: