JUKWAA la Wahariri (TEF), limelaani kitendo cha kuzomewa na kudhalilishwa kwa waandishi wa habari wa ITV, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, Oktoba 30 mwaka huu.
Akizungunza na waandishi wa habari Katibu wa Jukwaa hilo, Neville Meena amesema kuwa kitendo hicho si cha kukaliwa kimya kutokana na kukwaza utendaji wa kazi na kudhalilisha utu wa waandishi hao mbele ya jamii.
Meena amesema kuwa waandishi na wafanyakazi wa kituo hicho walikuwa katika ofisi hizo za CCM, wakirusha na kuandika habari za tukio la mapokezi ya Dk. John Magufuli baada ya kukabidhiwa hati ya ushindi wa urais na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika hafla iliyofanyika siku hiyo katika ukumbi wa Diamond Jublee.
“Kuzomewa kwa waandishi hao katika ofisi za CCM ni muendelezo wa kile kilichoanzia Diamond Jubilee ambapo wafuasi wa Chama cha Mapinduzi CCM, walionekana wakiwazomea wafanyakazi wa ITV na baadaye kumzonga Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk Reginald Mengi ambaye ni mmliki wa kituo hicho,” amesema Meena.
Ametoa onyo kwa kuwataka wafuasi hao waache vitendo hivyo, akisema kuwa utafiti mdogo waliofanywa na Jukwaa hilo kuhusu vitendo hivyo vinatokana na wafuasi hao kuchukizwa na jinsi kituo hicho kilivyoripoti, matukio ya kampeni na kuwapa fulsa wagombea wa vyama vingine vya siasa.
Amesema kuwa kituo hicho ni miongoni mwa vyombo vya habari vilivyofanya kazi zake kwa weredi wakati wa kampeni za wagombea wa vyama vyote nchi nzima ambapo Dk. Magufuli na Mgombea Mwenza, Samia Suluhu walikuwa na wandishi wa kituo hicho miongoni mwao ni Emmanuel Buhohera na Halfan Liundi ambapo umma wa watanzania ulipata kufahamu kinachoendelea katika mikutano yao ya kampeni.
Meena ameongeza kuwa hilo sio tukio la kwanza kufanywa na chama hicho kwani wakati wa kampeni za mgombea urais kilimfukuza katika msafara wa Dk. Magufuli mkoani Mbeya, mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Peter Elias kwa madai ya kutofurahishwa na habari aliyoandika kuhusu mgombea wao.
Amesema kuwa matuko hayo siyo ya kiungwana na hayatakubalika katika jamii ya watu wastaarabu. Ikiwa waandishi wa habari au vyombo vya habari vinafanya makosa zipo njia za kisheria za kushughulikia makosa hayo pamoja na kufanya mazungumzo kupitia taasisi za waandishi wa habari.
“Tunachukua fulsa hii kuvitaka vyama vya siasa kama taasisi viongozi, wanachama na wapenzi wake kuacha mara moja vitendo vya kuwashambulia waandishi wa habari kwa sababu zozote zile. Tusingependa ifike hatua kutangaza kwamba matukio ya chama fulani ni hatari kwa waandishi wa habari,”amesema Meena.
Kadhalika tunachukua fursa hii kuvitaka vyama vya siasa na watu binafsi wanaoandaa mikutano inayowahusisha waandishi wa habari kuhakikisha kuwa waandishi wanakuwa salama wanapo hudhuria kwenye mikutano yao na kuchukua hatua ya kukemea.
“Tunasikitika kwa ukimya wa chama hicho ulionyesha kufurahishwa kwa tukio hilo kutokana na kutotoa kauli yoyote,” amesema Meena.

8 comments:
Jambo muhimu linalopaswa kusisitizwa na kufundishwa kwa vijana kutokana na tukio au matukio haya ni umuhimu wa kuzingatia sifa za ueledi na taaluma (professionalism) katika utendaji wa kazi yo yote ile iwe ni utunzaji wa usafi katika majengo ya ofisi (janitorial) au uandishi wa habari (journalism). Vyombo vya habari vinapaswa kuonesha pande zote za stori - kisha katika uchambuzi ndipo chombo husika kinaweza kuegemea kwenye mrengo wake. Ninafikiri ITV walitimiza hilo kwa kiasi cha kuridhisha wakati wa kampeni lakini vyombo kama TBC1 walishindwa kuonesha kiwango cha taaluma. Utamaduni wa kuheshimu na kuzingatia taaluma unapaswa kuingizwa katika mitaala ya elimu angaa tuwaokoe watoto wetu wasije wakatumbukia kwenye ushabiki usiokuwa na tija ambao ndio unatupa shida katika kizazi hiki. Luke nifikishie maoni haya kwa waziri mpya atakayekabidhiwa wizara ya elimu.
CCM na wanaojiita wapenzi nadhani inafika pahali sasa tuelimike na ushabiki usiokuwa wa kistaarabu ukomeshwe. Waandishi waavhwe kuwapelekea wananchi kile kinacjotokea.
Hili ni Jukwaa la Wapumbavu!!! Anyway, let me pause and allow these stupid and corrupt journalists to exercise their freedom of expression. There's no doubt that even those CCM members being criticized here were just exercising their freedom of expression!!!
It's unconscionable that these idiots never raised their voice against the booing that was persistently done by UKAWA hooligans to anyone spotted in CCM attire on certain streets of Dar Es Salaam. Why didn't they call upon UKAWA to control their hooligans, but they expect CCM to restrain its members? Jukwaa la Wapumbavu, instead, thought such acts were just great newsworthy episodes!!!
Those ITV idiots, including their boss are hypocrites of the highest order. I'd say they reaped precisely what they had sowed. They shouldn't make no complaint!!!
Mdau wa 8:16pm... umeeleza ukweli kabisa wanavuna walichokipanda sasa kelele za nini ?
Ni jukwaa la wanafiki na wapotoshaji. Mengi na vyombo vyake vya habari mara kadhaa wakati wa kampeni vimekuwa vikitoa taarifa za uongo au kuzidisha chumvi ya ubaya kwa habari zilizohusu CCM na mgombea wake na hakuna aliekemea.
Vipi kauli za ukawa yakwamba walikuwa wakimzomea mgombea wa CCM na wakati mwengine kuweka kwenye yutube baadhi ya matukio hayo au kuripotiwa na magazeti ya ipp kwamba magufuli kazomewa vipi wahariri walishindwa kulaani na hilo la kumzomea magufuli ni hatari zaidi kwani Magufuli alikuwa na watu wake wakuweza kujibu mapigo na ikawa balaa kuliko huyo mengi hana nguvu ya umma yoyote iliokuwa nyuma yake inayomsapoti kuzomewa kwake ni sawa tu hata angelichapwa basi kesi ingeishia police tu bila ya kuhatatisha amani ya nchi tofauti na magufuli kama wafuasi wake wangeamua kuingiana maungoni na waliokuwa wakijaribu kumdhalilisha mgombea wao kwa kweli nchi ingewaka moto wahariri hawakuliona hilo?. Tunaomba wahariri wawe fair sio fare kwa maana ya kununuliwa na wenye pesa ili watoe taarifa za kipuuzi.
JUkwaa kama jukwaa lapaswa kutokuegemea upande wowote ule.Walipaswa kutoa maoni yao kwa mwenendo mzima wa uandishi wa habari wakati wote wa uchaguzi na hapo ndo watoe maoni yao na kutoia mifano na sio kusubiri mpaka boss wake afanyiwe kitendo ndo waje na hizi taarifa za kulaani,mbona kuna waandishi wa vyombo vya habari wameumizwa na kuharibiwa vitendea kazi vyao na wanachama wa chama fulani lakini hamkutoa taarifa ya kulaani??.Jambo lingine ni kwenu ninyi waandishi japo mwajitahidi lakini mara nyingi huwa mnaonyesha mapenzi yenu dhahiri kitu ambacho si kizuri hata kidogo,mnabidi kujiepusha na ushabiki wa pande yoyote ile
Ni vizuri amejionea kuwa panapokosekana heshima, upendo na amani hakuna aliye salama.
Well stated by Anonym. @8:16 PM! Wadau, make no mistake, it is a well established fact, Mr. Mengi is the number one supporter and financier for the opposition Ukawa/Chadema. His media empire was 100% behind all the misinformation played out during the presidential campaign. Give us a break Mr. Meena, don't hide behind the cover of TEF to conceal your true ideology. We know that you are pro-Ukawa/Chadema, and the views expressed are Chadema's and not TEF's. You are not impartial in this regard, and don't play Mr. Niece Guy because you are a typical "FOR SALE" JOURNALIST/EDITOR just like many others at TEF.
Kama alikuwa napendelea upande mmoja wacha AZOMEWE. Hata hapa USA wanahabari wa CNBC wanakosolewa na kuzomewa kwa maswali yao ya bias zidi ya GOP.
Post a Comment