ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 4, 2015

SIKU YA MWISHO YA RAIS KIKWETE IKULU TUPIA NENO LAKO KWA MH.RAIS BILA KUMDHIHAKI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifanya kazi ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam kwa mmara ya mwisho leo Novemba 4, 2015 kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais wa awamu ya Tano anayetarajiwa kuapishwa kesho Dkt John Pombe Joseph Maguful.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoka ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kufanya kazi katika siku ya mwisho leo Novemba 4, 2015 kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais wa awamu ya Tano anayetarajiwa kuapishwa kesho Dkt John Pombe Joseph Magufuli.

9 comments:

James Bond said...

Sasa Kama Mtoa hoja unaomba maoni ya watu kwa nini unatusihi tuseme unavyotaka wewe? Kama Unataka kufurahisha watu ungetumia MIchuzi blog...Kikwete ametuachia deni kubwa Sana Tanzania na anaingia Kwenye history ya viongozi wengi wa KiAfrica wasiopenda demokrasia ,Hali ha ZNZ ni tete, Nchi inahitaji katiba mbadala Lakini kwa mapenzi ya CCM Kikwete alifunika maslahi ya taifa..Kwaheri mtalii watu uliemshinda hata Nyerere kwa Safari lukuki zisizo na tija kwa taifa..

Anonymous said...

Bado dunia inakuhitaji. Tunakushukuru kwa
mchango wako mkubwa wa kipekee.
Ubarikiwe na maisha marefu zaidi, afya njema,
na amani. Na bado.

Unknown said...

Mueshimiwa kikwete ni moja ya mwanadiplomasia wa kweli chini ya uongozi wake Tanzania inaheshimika zaidi duniani kwa Tanzania itakosa jembe la uhakika katika anga za kimataifa. Kwa nyumbani upanuzi wa kidemokrasia wa mtu kuelezea hisia zake umekuwa hauna kifani sidhani kama kuna nchi Afrika inaizidi Tanzania . Kimaendeleo Tanzania ni dhahabu iliokuwa ishachimbwa inahitaji kushafishwa tu. Kwa maana hiyo Tanzania ni ambayo wakati wowote itauaga umaskini na ujio wa tinga tinga utamaliza ubishi kabisa. Hao wpinzaani waache waendelee kutoa tarifa za uongo lakini ukweli halisi unajulikana, chadema wamezoea uongo, uzushi, ujinga hadi kuwatia upofu wa akili wafuasi wao kiasi kwamba wamekuwa mazezeta yasio jua mbele wala nyuma. Hongera kikwete kwa kwa utumishi uliotukuka tunakutakia mapumziko mema na maisha ya furaha amen.

Anonymous said...

Usisahau kutaja mali zako muheshimiwa !

Anonymous said...

Without sugarcoating JK 2-terms was so corrupted than any other presidency terms since independence. He erupted nation debt from 9 trillion when he took the office to 40 trillion now. If father of the nation the original and the great JK Nyerere was alive he couldn't become a president of our great nation. May God rest his soul in eternal peace amen. The statistically he has been abroad equivalent to 2 years of his presidency that will be sufficient to take care of poor health and education problem for the entire country. please post this comment and allow my freedom of speech.

Anonymous said...

Mimi ninafikiri mazezeta wakubwa ni wale wanaoichagua chama kilichoinyonya nchi nzuri ya Tanzania kwa zaidi ya miaka 54. Bado Tanzania iko na huduma duni za afya, elimu, bara bara mbaya, ufisadi ulio kubuhu, ajira duni kwa vijana, utapanywaji wa mali asili ya nchi, sera mbaya na mfumo mbovu wa katiba unaoifanya chama tawala kutawala kwa mabavu.

Anonymous said...

Mimi nilikuwa Rwanda na hatimaye Kosovo. Nasema kwa majivuno kuwa mgombea wangu ameshinda na alichukua madaraka (majukumu yake) kwa mbwembwe kabisa. Namshukuru Kikwete kwa mchango wake katika kumlea mgombea huyu na kumpigia kura kwa mara nyingine uchaguzi huu. Mgombea huyo au Mshindani huyo (kama alivyosema) leo Mhe. Rais Magufili ni AMANI. AMANI AMANI AMANI. M/Mungu azidi kumlinda na kutudhihirishia thamani yake mgombea huyu. Ikishakuwa na huyu, "_KAZI TU" inawezekana. May Peace prevail.

Anonymous said...

Life will pay what you ask for... if you plant oranges expect them in the future not otherwise.

Anonymous said...

Tunakushukuru, kutukabidhi nchi yetu ikiwa salama. Nenda kapumzike kwa amani. Asante.