Advertisements

Sunday, November 29, 2015

KFC WAFUNGUA MGAHAWA MPYA ENEO LA KARIAKOO JIJINI DAR

Mkurugenzi mkuu wa KFC nchini Tanzania, Louis Venter(kushoto) akikata utepe wakati wa ufunguzi wa tawi la KFC eneo  la Kariakoo jijini Dar ambapo waliweza kusherekea na watoto wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi ya Uhuru Mchanganyiko.
Mkurugenzi mkuu wa KFC nchini Tanzania, Louis Venter akiwakaribisha wageni waalikwa pamoja na kuzungumza jambo wakati wa ufunguzi wa Mgahawa wa KFC eneo la Kariakoo jijini Dar.
Mkurugenzi mkuu wa KFC nchini Tanzania, LOuis Venter(katikati) akimkabidhi hundi ya Shilingi milioni Moja Mwalimu mkuu Msaidizi wa shule ya Uhuru Mchanganyiko wakati wa ufunguzi wa Mgahawa huo hii ikiwa ni kutoa mchango kwa jamii hasa kwa watotot wenye mahitaji maalum.
Mkurugenzi mkuu wa KFC nchini Tanzania, Luis Venter(kushoto)  akiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya wanafunzi pamoja na waalimu wa shule ya Uhuru Mchanganyika wakati wa ufunguzi rasmi wa Mgahawa wa KFC eneo la Kariakoo jijini Dar
Mmoja wa wahudumu hao akiwahudumia wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu mara baada ya ufunguzi wa Mgahawa huo eneo la Kariakoo jijini Dar
Mkurugenzi mkuu wa KFC nchini Tanzania, Luis Venter akitoa huduma kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum mara baada ya ufunguzi wa Mgahawa huo.
Wanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko wakiendelea kupata chakula uku wakisimamiwa na walimu wao kushoto ni Mwalimu Upendo Andrew na kulia ni Mwalimu Julius Mganda aliyesimama
Wafanyakazi wa KFC tawi jipya la Kariakoo wakitoa burudani kwa wageni waalikwa waliofika katika ufunguzi wa mgahawa huo.

No comments: