Katika Mkuu wa CUF Mhe.
Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na viongozi wa Wilaya na Majimbo wa Chama
hicho katika Ukumbi wa Majid, Kiembesamaki Zanzibar.
Mwenyekiti wa kamati ya Uongozi CUF
Taifa Bw. Twaha Taslima, akisoma maazimio ya baraza kuu kwa waandishi wa habari
katika ofisi za Chama hicho Vuga mjini Zanzibar.
Viongozi wa Wilaya na
Majimbo wa CUF, wakimsikiliza katiba mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif
Sharif Hamad katika Ukumbi wa Majid, Kiembesamaki Zanzibar.(Picha na Salmin Said, OMKR).
Na: Hassan Hamad, OMKR
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka
wafuasi na wapenzi wa Chama hicho kutembea kifua mbele kutokana na ushindi
mkubwa walioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 mwezi uliopita.
Amesema
ushindi huo umeleta matumaini mapya kwa wazanzibari ambao wameitumia vyema haki
yao ya kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaoataka.
Akizungumza
na wajumbe wa mkutano mkuu ngazi za Wilaya na Majimbo katika ukumbi wa Majid
Kiembesamaki Zanzibar, Maalim Seif amesema hakuna namna yoyote ya kupindua
maamuzi ya wananchi waliyoyafanya kupitia masanduku ya kura.
Amesema
wanachokifanya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar hivi sasa ni kuchelewesha
kukamilisha uhakiki wa kura kwa majimbo 14 yaliyobakia na kumtangaza mshindi wa
Urais, na hivyo kuishauri tume hiyo kukamilisha zoezi hilo ili serikali mpya
ianze kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi.
“Mimi
sina wasi wasi, ninajihesabu kama Rais ninayesubiri kuitwa na kuapishwa, na
sasa nimo katika matayarisho ya kuunda serikali ili nikiapishwa tu nisipoteze
tena muda wa kufikiria kuunda serikali”, alisema Maalim Seif katika kikao hicho
cha kwanza cha kuzungumza na wajumbe hao tangu uchaguzi mkuu wa Zanzibar
ulipomalizika.
Amesema
tayari dunia nzima wanamfahamu Rais aliyechaguliwa na wananchi wa Zanzibar
katika uchaguzi mkuu uliopita, na kuwataka wanachama wa Chama hicho kuacha
kusikiliza kile alichokiita proganda za Chama Cha Mapinduzi zinazoeleza
kurejewa kwa uchaguzi.
Amefahamisha
kuwa hakuna sababu za kurejewa kwa uchaguzi huo kwani uchaguzi ulishakamilika
katika ngazi zote na washindi wa uwakilishi na udiwani kutangazwa bila ya
kuwepo malalamiko yoyote, na kwamba kinachosubiriwa hivi sasa ni kukamilika kwa
zoezi la uhakiki wa kura za Urais kwa majimbo yaliyobakia na hatimaye mshindi
wa uchaguzi huo aweze kutangazwa.
Akizungumzia
madai ya ongezeko la kura katika kisiwa cha Pemba, Maalim Seif amesema madai
hayo hayana ukweli kwani hakuna hata kituturi kimoja kilichozidishwa wapiga
kura 350 kiliwopangiwa na kwamba vituturi vingi vilikuwa na wapikura chini ya
idadi hiyo.
Mapema
akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mipango na Chaguzi wa CUF Omar Ali
Shehe, amesema licha ya ushindi wa Urais, Chama hicho pia kimepata ushindi
mkubwa kwa nafasi za Uwakilishi na Udiwani.
Amesema
katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Chama hicho kilipata Wawakilishi wanne (4)
na madiwani saba (7) kwa upande wa Unguja ambapo uchaguzi wa 2015 kimefanikiwa
kupata Wawakilishi tisa(9) na madiwani kumi na tano (15).
Aidha
amesema Chama Cha Mapinduzi kimepoteza wodi zote tatu (3) za udiwani katika
kisiwa cha Pemba na kukifanya Chama hicho kushindwa kupata mjumbe yeyote wa
Baraza la Wawakilishi, Ubunge na Udiwani.
Kabla ya
mkutano huo, Baraza Kuu la Uongozi CUF chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama hicho Taifa Bw. Twaha Taslima,
liliitisha mkutano wa waandishi wa habari kueleza maazimio ya baraza hilo
kufuatia kikao chake cha dharura kilichokutana jana 07/11/2015 katika hoteli ya
Mazsons Mjini Zanzibar.
Katika
maazimio yake Chama hicho kimeishauri Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)
kutengua uamuzi wa mwenyekiti wake Bw. Jecha Salim Jecha wa kufuta uchaguzi
mkuu wa Zanzibar, kwa vile hana mamlaka ya kikatiba na sheria ya uchaguzi
kuweza kufuta uchaguzi huo.
5 comments:
NYIE CUF MWATAFUTA TU VURUGU, KUMBUKENI YUKO MWANAUME WA SHOKA MAGUFULI , AKIAMUA KU MAGUFULIKA NDIO MTAIPATA
Kwa hali ilivyo sasa hivi sioni namna yoyote ile ya kutatua huu mgogoro isipokuwa kwa kuweka serikali ya mpito.Serikaki ya mpito si ajenda ngeni Zanzibar.
Seif alishinda, CCM wameona wameshapoteza urais wameona wauvuruge uchaguzi. Hilo halikubaliki. Sasa uchaguzi umefanyika wa nini kama mnakataa kukabidhi serikali? Wewe hapo juu unayesema Magufuli atawaumiza, naomba uongeze uwezo wako wa kufikiri.
kama Lowasa na Chadema, Bw. Seif anayo njaa kubwa ya Urais. Anataka kuwa Mfalme wa Unguja by any means necessary. The question is; KWELI ATAFANIKIWA wakati Brigedi nzima ya NYUKI imejiandaa?
CUF Ni Wadini wakubwa lugha na sera zao zimejaa udini
Post a Comment