Advertisements

Friday, November 27, 2015

TIGO YADHAMINI ONESHO LA MWANAMUZIKI MOUSSA DIALLO KUTOKA NCHINI MALI

Meneja wa Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo, John Wanyanja (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu kampuni hiyo kudhamini onesho la mwanamuziki Mousa Diallo kutoka nchini Mali lililofanyika katika Mgahawa wa Chakula na Vinywaji wa Samaki Samaki, Masaki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Masoko wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Saum Wengert na katikati ni Mwanamuziki, Moussa Diallo.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo, John Wanyanja (kushoto), akizungumza na Mwanamuziki, Moussa Diallo (kulia). Katikati ni Mmiliki wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Carlos Bastos.
Mwanamuziki Moussa Diallo wa nchini Mali anayeishi Denmark (katikati), akiimba mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam  wakati akijitambulisha ambapo alifanya onesho lake Ukumbi wa Samaki Samaki, Masaki jijini Dar es Slaam. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo, John Wanyanja ambao wamewezesha ujio wa mwanamuziki huyo na kushoto ni Ofisa  Mkuu wa Masoko wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Saum Wengert.
Ofisa Mkuu wa Masoko wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Saum Wengert (kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu onesho hilo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Warembo wa Samaki Samaki wakifuatilia matukio mbalimbali ya mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale



MWANAMUZIKI maarufu toka Afrika Magharibi anayeishi Denmark, Moussa Diallo, jana Novemba 26, 2015 alifanya onesho lake katika Mgahawa wa Chakula na Vinywaji wa  Samaki Samaki uliopopo Masaki jijijini Dar es Salaam lililoenda sanjari na ziara ya kutembelea  miradi mbalimbali ya kijamii hapa nchini.



Onesho hilo lililodhaminiwa na Kampuni  ya simu za mikononi ya Tigo ikishirikiana na Mgahawa huo wa  Samaki Samaki lilifanywa na Mwanamuziki huyo toka nchini Mali mwenye asili ya Denmark, ambaye amewasili nchini siku ya Jumatano Novemba 25, 2015.



 Akizungumza Dar es Salaam asubuhi kwenye mkutano wa waandishi wa habari, Ofisa Mkuu wa Masoko wa Samaki Samaki, Saum Wengert, alisema mwanamuziki huyo anapiga muziki wa aina ya soul iliyochanganywa na vionjo vya kiafrika na muziki wa Magharibi unaopendwa ulimwenguni kote.



 Alisema onesho hilo pia linatarajiwa kufanyika leo  (Novemba 27) katika Hoteli ya Melia jijini Zanzibar na baadae watafanya Full Moon Party kwenye Hotel ya Kendwa Rocks iliyopo jijini Zanzibar. 



Moussa alizaliwa jijini Paris nchini Ufaransa na kukulia Bamako nchini Mali ambapo hivi sasa anamakazi yake Copenhagen nchini Denmark.



Katika juhudi za kukuza utamaduni, Diallo anachanganya muziki wake kwa kushirikisha vikundi mbalimbali vya utamaduni ikiwemo; Dawda Jobarten (Kora, Mwimbaji), Preben Carlsen (gitaa), Salieu Dibba (Percussions, Sauti), na Marco Diallo (Ngoma).



Kwa upande wake, Meneja uhusiano wa Tigo, John Wanyacha alisema kampuni hiyo na wadhamini wengine wamekubali Diallo kufanya onesho nchini ikiwa ni pamoja na kuweka mahusiano mazuri yaliyopo na maonesho yanayokuja.



Alisema kuwa wanafahamu wanachopenda wateja wao kwenye muziki na kwamba wana eneo ambalo linaweza kuwawezesha kuzuia miziki wasioyoipenda hivyo ujio wa Diallo nchini utaendeleza makubaliano mazuri kati ya kampuni hizo kwa kuwapa wateja wanachokihitaji ikiwa ni pamoja na vionjo. 


Wengine waliodhamini ziara hiyo ni pamoja ni; Johnnie Walker, French Kiss, Heineken na Ledger Plaza Bahari Beach.




No comments: