ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 23, 2015

Wabunge CUF wamshukia Ndugai

(CUF) wamemtuhumu Spika wa Bunge, Job Ndugai kumruhusu Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kuingia bungeni.

Kwa mujibu wa wabunge hao, Spika alifanya bhivyo licha ya wao kupinga hatua hiyo.

Vilevile, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), ametangaza kumfikisha mahakamani Spika Ndugai akidai kwamba alikiuka taratibu na kanuni za Bunge kwa kuwatoa nje wabunge wanaounda Umoja ya Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Wabunge hao pia wamemtuhumu Ndugai kwa kuwaingiza katika ukumbi wa Bunge zaidi ya polisi 40 kinyume cha sheria.

Hayo waliyasema walipozungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya CUF, Buguruni Dar es Salaam jana.

Walisema katika hali ambayo hawakuitarajia, viti ambavyo hutumiwa na wabunge wa upinzani vilitolewa sehemu ya kukanyagia kwa hofu kwamba wangevitumia kuleta fujo.

Mwenyekiti wa wabunge hao, Juma Hamad Omar, alisema kabla ya uzinduzi wa Bunge kufanywa na Rais Dk. John Magufuli, walimwandikia Spika Ndugai barua kuhusu msimamo wao wa kutotaka Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, aingie ndani ya ukumbi wa Bunge.

Alisema licha ya kumwandikia barua pia walipata fursa ya kufanya naye mazungumzo kwa takribani saa moja juu ya suala hilo.

Pamoja na juhudi zote hizo, Spika Ndugai alionekana kutotaka kuwasaidia akisema kuwa yeye uwezo wake ni kumfikishia ujumbe Dk. Shein na kwamba mambo mengine hana uwezo nayo.

Juma alihoji kwa nini kiongozi huyo wa Bunge ashindwe kutumia mamlaka yake na badala yake afanye uamuzi kwa kushauriana na mhimili mwingine wa Serikali.

Alisema wabunge wa CCM Zanzibar walikataa Makamu wa Kwanza wa Rais wa visiwa hivyo, Maalimu Seif Sharif Hamad asiingie ndani ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi siku baraza hilo lilipovunjwa na amri hiyo ilitekelezwa.

“Sasa yeye kwa nini ashindwe kutumia mamlaka yake na wakati wale ni waalikwa tu? Matokeo yake akaja kumuingiza mpaka Spika wa Baraza la Wawakilishi ambalo kwa sasa halipo.

“Na wakati akitengua kanuni ili hawa waingie, Tundu Lissu alipinga lakini spika kwa ubabe akapitisha,”alisema Juma.

Alisema kutokana na mambo hayo, Ndugai ndiye aliyemvunjia heshima Rais Dk. Magufuli kwa kushindwa kuwasikiliza wabunge wake ambao waliamua kupiga kelele na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.

Mnadhimu wa wabunge hao, Ali Salehe, alisisitiza viongozi hao waliingizwa bungeni kinyume cha sheria.

Alisema Spika bila kuwaombea kibali kama kanuni zinavyotaka, aliruhusu zaidi ya polisi 40 kuingia ukumbini lengo likiwa ni kupambana na wabunge wa upinzani.

Alisema baadhi ya askari hao walikuwa wamevaa sare na wengine walikuwa na nguo za raia na walikuwa wamepangwa kila askari mmoja apambane na wabunge wanne wa upinzani.

“Lakini pia hata viti vya wapinzani na vile vya wabunge wa CCM vilikuwa tofauti.

“Kwenye vile vyetu walikuwa wametoa sehemu ya kuwekea miguu wakidhani tungeitumia kurusha wakati ambao tungefanya fujo kumbe sisi hatukuwa na mpango wa kufanya fujo,” alisema Salehe.

Wabunge hao walisema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limezinduliwa na rais likiwa halijakamilika.

Alisema kwa mujibu wa sheria Bunge hilo linatakiwa kuwa na wabunge watano kutoka Baraza la Wawakilishi ambao mpaka sasa hawapo kwa sababu uchaguzi wao umetangazwa kuahirishwa.

Kutokana na mambo hayo, wabunge hao walisema Zanzibar hakuna mgogoro wa siasa na kwamba CCM wanasema hivyo kuhalalisha mambo yo.

“Kwa hiyo tunataka mchakato ukamilishwe na mshindi atangazwe ili pia kuhalalisha ushindi wa Dk. Magufuli ambaye alipigiwa kura na watu walewale waliompigia Maalimu Seif,” alisema.

Alisema Wazanzibari wamechoka kusubiri, na kuendelea kuliweka taifa hilo kwenye taharuki ni kuhatarisha amani ya nchi.

MTANZANIA jana ilimtafuta Spika Ndugai kuzungumzia madai hayo lakini hakupatikana.

Hata hivyo alipoulizwa, Ofisa habari wa Bunge, Owen Mwandumbiya, alipuuza madai ya wabunge hao kuhusu kilichotokea bungeni akisema wanajaribu kutengeneza kitu ambacho hakikuwapo.

Kubenea kutua kortini

Wakati huohuo, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, amesema anatarajia kumpeleka mahakamani Spika wa Bunge, Job Ndugai akidai amekiuka taratibu na kanuni za Bunge kwa kuwatoa nje wabunge wanaounda Ukawa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dodoma jana, Kubenea alisema Ndugai alivunja kanuni na taratibu za Bunge kwa kuwatoa wabunge wa Ukawa nje kwa sababu walichokuwa wakikidai ni halali.

Alisema kile walichokuwa wakikidai kuwa Rais wa Zanzibar Dk Shein hatakiwi kuingia bungeni ni kweli ikizingatiwa aliingia Novemba 3 mwaka 2010 na ukomo wake ulikuwa ni 2 Novemba 2015.

“Spika anasema mpaka Rais atakapopatikana ndiyo unakuwa mwisho wa Rais wa Zanzibar, siyo kweli.

“Ukomo wa Rais wa Zanzibar uliishakoma na katiba zetu za Tanzania na Zanzibar zinasema ndani ya miaka mitano au ukomo wa vipindi viwili visivyozidi miaka 10,’’ alisema.



Kubenea alisema atampeleka mahakamani Ndugai akishirikiana na wakili wake, Peter Kibatara.

“Ndani ya wiki hii tunaenda mahakamani. Job(Ndugai), amevunja taratibu na kanunu za bunge na kulinajisi kwa kumruhusu Dk. Shein kuingia bungeni.

“Tunamshitaki kwa kuvunja kanuni na taratibu, tumeshauriana na mwanasheria wangu tunaenda mahakamani,’’ alisema

Mbunge huyo ambaye ni mwanahabari mashuhuri, alishangazwa na hatua ya Spika Ndugai kuwaruhusu Polisi na Usalama wa Taifa kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu na kanuni zinazoendesha mhimili huo.

“Wale askari waliandaliwa kwa ajili ya kutupiga na walipania kutupa mkong’oto.

“Sasa sisi tuna wabunge walemavu tuliogopa tukaamua kutoka nje, kitendo kile kimelivunjia hadhi Bunge na nchi inayojiita yenye utawala bora.

“Nasema hivi Ndugai hana uwezo wa kulidhibiti Bunge wala kutuzuia sisi, tena tunamuonya mapema hawezi kuuzima huu moto huu,’’alisema Kubenea.

Mtanzania

10 comments:

Anonymous said...

being member of parliament doesn't mean that you are that much free to such not listen even to the speaker!at that position you do no represent your self,but you are presenting,and you are working for the people who voted with a greater number from your area.shortly,we were ,and we not interested with what you did on the first speech that was presented to you by the president of Tanzania.you real made us feel sorry to our president as you misrepresented us!we have no interest on what you did.we are poor,we have a lot of problems,we need peaceful changes,and not what you did!now how do you feel after listening from outside the building the good speech presented by the president?it is shame upon you!now you are going to discuss on his speech!you please see your self!kubenea,its your first time to get that position,you please work for the people,do not work on self interest that doesn't help solve our problem.you talk much.it is not how many people hear your voice but what you deposit for our development!just finetunne your self..you need to change mazee

Anonymous said...

mimi kwa kweli nilimpigia kura mbunge wa Ukawa, sasa hivi najuta kwa kweli na wanapotupeleka, badala ya kumsikiliza Raisi kwanza na anachopanga kwa ajili ya nchi yetu, wao wanatuvuruga, kama kweli ukawa wanaona wanaonewa na serikali ya mapinduzi zenji, basi sheria ianze kufuata mkondo wake, maalim seif alijitangazia ushindi kabla hata kura hawajamaliza kuhesabu yeye awe wa kwanza kupelekwa mahakamani, na sheria zingine zifuate, wasiangalie upande mmoja tu kila siku wao wanaonewa wakati wanavunja sheria, sisi tumewachagua mtuleteee maendeleo na kama ni kupambana na sheria mzifuate sio kufanya fujo, matokeo yake mmetolewa hakuna mlichopata, msonyoooo

Anonymous said...

Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, Dr.Shein bado ni raisi halali wa Zanzibar mpaka pale raisi mteule atakapoapishwa.Je,CUF wanatambua kuwa Maalim Seif bado ni makamu wa kwanza wa raisi? Hatujasikia kauli ya maalim Seif kujiuzulu wadhifa wake..Hivyo wanapaswa kumshangaa maalim Seif kwanza kabla ya kuhoji uwepo wa Dr.Shein kwenye bunge..

Anonymous said...

Bila shaka mtu aliyetoa comments hizo hapo juu namba 1- 3 ni huyo huyo mmoja, na anaonyesha ni mkereketwa haswa wa CCM!! Ni huyo huyo kwa kuwa kuna ushahidi wa kimaandishi neno, "Rais" anasema "raisi". Shule pia inaonekana imempiga chenga kidogo, maana Kiingereza kinachobomolewa kwenye comment ya kwanza ni balaaa!! Jamani Wabongo, acheni kutafuta vyeo kwa njia za mkato, kuonyesha ushabiki na ukereketwa wa kupindukia,ili uonekane na wakubwa wakufikirie kukupa cheo au ulaji! Jamani nendeni shule halafu mpate ajira nzuri za halali kulingana na uwezo wenu wa kielimu na kitaalamu(academic and professional merit).

Anonymous said...

Anonymous namba mbili unazungumzia sheria gani wakati sheria na kanuni tayari zimeshavunjwa kuanzia Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Spika wa Bunge na serikali ya JMT ambayo haitaki kusikiliza maoni au mtizamo tofauti na wanavyotaka wao. Kesi ya ngedere unampelekea nyani...unajua matokeo yake. Kama Magufuli ameamua kufumbia mmacho suala la Zainzibar na kuziba masikio kama kwamba kila kitu ni shwari, basi awe tayari kupambana na shubri na vuguvugu la takribani nusu ya Wazanzibari ambao wana hisia tofauti na zile za Chama cha Mapinduzi. Ni vyema alivalie njuga sula hili alishughulikie kiungwana na kulimaliza badala ya kuficha kicwa ardhini na kusema hakuna tatizo. La sivyo, kipindi cha miaka mitano ijayo kitakuwa kigumu sana kwake, kwa polisi, wanausalama na kwa CCM. Solve the Zanzibar political impasse and paralysis first, then the country can move foward on other issues!

Anonymous said...

The legislators from the opposition camp are thugs and hooligans who hardly know or completely ignore the real reasons why their poor voters sent them to the legislative body. This is utter disservice to their constituencies!

Anonymous said...

CCM ndiyo ipo madarakani, kama CUF na gang yenu ya Ukawa hamtaki kuongozwa na bunge la CCM basi acheni kazi, la sivyo endeleeni ili muwawakilishe wananchi bila fujo.

Anonymous said...

Acha kutishia serikali nyau...

Anonymous said...

Jibu au changia hoja, hapa Hatuhitaji a forensic analyst .

Anonymous said...

wewe anonymous wa 5:25pm mburura kweli nani ambaye anataka cheo mbona hatuoni jina. acha zako kula ndimu uchaguzi umeshaisha sisi tunajenga nchio wewe kaaa kulalama kama wale wale walitoka. wewe unasema eti kiingereza kibovu!! wewe Kiswahili kinashinda kuandika, utawajua watu wa ukawa< hivi ukawa ndiyo nini tena msaada tutani wajameni.