Advertisements

Saturday, November 21, 2015

Waziri mashuhuri Kenya Anne Waiguru ajiuzulu-BBC

WAIGURU TWITTERImage captionWizara ya ugatuzi imekabiliwa na tuhuma nyingi za ufisadi karibuni

Waziri mwenye ushawishi mkubwa katika serikali ya Rais Uhuru Kenyatta amejiuzulu wadhifa wake baada ya shinikizo kutolewa ajiuzulu kutokana natuhuma za ufisadi.

Bi Anne Waiguru, ambaye amekuwa Waziri wa Mipango na Ugatuzi, ameambia wanahabari Nairobi kwamba ameshauriwa na daktari wake “achukue muda kupumzika”.

Amewaambia wanahabari kwamba amemwandikia Rais Kenyatta akimtaka amuondolee majukumu yake.
Wakenya wapigania waziri kwenye Twitter

Hata hivyo amesisitiza kwamba hana hatia.

“Ninafuata ushauri wa daktari na nimemuomba Rais aniondolee majukumu yangu kama waziri ... na akiona inafaa, anipe majukumu ambayo si mazito,” Bi Waiguru amesema.

No comments: