ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 26, 2015

WIZARA YA MAMBO YA NJE YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 45 YA TAIFA LA OMAN


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akitoa hotuba wakati wa Maadhimisho ya miaka 45 ya Taifa la Oman yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Oman hapa nchini na kufanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) tarehe 24 Novemba, 2015. Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Salim Ahmed Salim. Katika hotuba yake Balozi Yahya alisifu uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Oman na kuitakia heri nchi hiyo katika kuadhimisha miaka 45.
Balozi wa Oman hapa nchini, Mhe. Soud Al Mohammed Al-Ruqaish akitoa neno la shukrani kwa wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 45 ya Taifa la Oman. Pia alisifu ushirikiano kati ya Tanzania na nchi yake na kuahidi kuuendeleza na kuuimarisha. 
Mhe. Mwinyi (wa kwanza kushoto) kwa pamoja na Mhe. Salim (wa pili kushoto) na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf (wa pili kulia) wakiwa kwenye sherehe hizo pamoja na wageni wengine waalikwa. 
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima (kulia) akiwa na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Tahir Khamis (mwenye suti ya kijivu) pamoja na wageni mbalimbali walioshiriki maadhimisho ya Miaka 45 ya Taifa la Oman. 
Kiongozi wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Balozi Juma Halfan Mpango (kushoto mwenye suti ya kijivu) akiwa na Balozi wa Burundi hapa nchini, Mhe. Issa Ntambuka wakati wa maadhimisho ya sherehe ya miaka 45 ya Taifa la Oman. 
Balozi wa Oman, Mhe. Al-Ruqaish akiwaongoza Viongozi Wastaafu, Mabalozi na Mgeni rasmi Balozi Yahya kukata keki kama ishara ya kusherehekea siku hiyo kubwa kwa Taifa la Oman. 
Wageni waalikwa wakifuatilia sherehe hizo akiwemo Afisa Mambo ya Nje kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Batholomeo Jungu (mwenye suti ya kijivu) 
Maafisa Mambo ya Nje wakifuatilia sherehe za miaka 45 ya Taifa la Oman. Kutoka kulia ni Bw. Ali Ubwa, Bw. Seif Kamtunda na Bw. Hangi Mgaka. 
Mhe. Mwinyi akijadili jambo na Mhe. Salim kabla ya kuanza kwa sherehe hizo za miaka 45 ya Taifa la Oman 
Picha ya Juu na Chini ni Sehemu ya Wageni waalikwa wakati wa sherehe za miaka 45 ya Taifa la Oman 
Sehemu nyingine ya Wageni waalikwa 





Wageni waalikwa



No comments: