Thursday, December 10, 2015

ALL THINGS AFRICAN” WALIVYOIPAMBA SHOO YA LADY JAYDEE LONDON

Si wengi wanaifahamu All Things African. Kampuni hii ndogo ya wanawake Uingereza imeanza kujenga jina kutokana rangi zake zenye bendera ya Tanzania na wanawake wachapa kazi wanaoongozwa na Hamida Mbaga. Jumamosi tarehe 5 Desemba 2015, All Things African, iliyapamba mazingira ya maonesho yake mwanamuziki Lady JayDee alipotumbuiza holi la Oasis, kitongoji cha Barking , mashariki ya London. Maonesho hayo yalitayarishwa na Upendo Events. Ushirikiano wa makampuni haya mawili unadhihirisha dira ya ushirikiano baina ya Watanzania ughaibuni. Hali kadhalika wakati wa karamu ya kusheherekea miaka 40 kati ya Tanzania na Uingereza (British Tanzania Society) All Things African ilikuwa na meza yenye bidhaa mbalimbali za Kitanzania na Afrika mjini Reading. Habari na picha na 
Freddy Macha

No comments: