Mwanaume mmoja ambaye amejulikana kwa jina la Geofrey Mhongole (37), amekutwa ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mwili wake kuwekwa nyuma ya gari lake lenye namba za usajili T850ACC aina ya Toyota Mark II.
Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Ramadhani Mungi, alisema mauaji hayo yalitokea Novemba 28, mwaka huu saa 11.00 alfajiri eneo la TRM-Minyarani Kihesa, Manispaa ya Iringa. Kamanda Mungi alisema baada ya polisi kupata taarifa, walikwenda eneo lilipotokea mauaji hayo ambapo walipofanya uchunguzi wa awali, walibaini kuwa Mhongole aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na watu wasiofahamika.
1 comment:
hii ni hatari kwa nchi yetu, na utaona polisi pamoja na kupewa magari lukuki kutakuwepo na ukimya mkuu hakuna uchunguzi wa dhati na marehemu atazikwa mara moja. Ni wakati wa kupiga vita mauaji ya kinyama namna hii kama yake ya Mawazo kule Geita ni kwa nini wahusika wasipatikane wakati wapo? Inteligencia ya polisi ikoje? kuna njia nyingi sana za kugundua maovu haya kwani mara ya mwisho alionekana akiwa na watu gani au mahali gani au anapenda kukaa maeneo gani? je walizozana au kugombana na nani siku za usoni yapo mengi yakufuatilia na polisi watende haki ili mahakama nayo iiweze kutoa haki au hukumu ilinganayo.
Post a Comment