Advertisements

Tuesday, December 1, 2015

January: WanaCCM msilalamikie kasi ya Rais Magufuli



January Makamba
By Ephrahim Bahemu, Mwananchi

Dar es Salaam. Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga, January Makamba amesema wanachama wa chama hicho watakaoguswa na kasi ya utendaji wa Rais John Magufuli, waache kulalamika kwa sababu ana lengo la kuijenga Tanzania mpya.

Katika taarifa yake ya chama kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana, Makamba alisema wapo wanaCCM maslahi yao yatagushwa na kasi hiyo, hivyo wasilalamike bali wakae na kujitathimini kama walichokuwa wakikifanya kina faida kwa Taifa na Watanzania.

Alisema kinachotakiwa kwa sasa ni kwa kila mwanachama kuunga mkono kila hatua anazochukua Rais Magufuli za kutaka kuleta mabadiliko ya kweli yanayotakiwa na Watanzania wote.

“Tusikae kimya, hii ni vita ninaamini Watanzania wote wanamuunga mkono lakini kwa kuwa anatekeleza ahadi za chama chetu, tunatakiwa kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono kwa kauli na vitendo,” alisema Makamba.

Alisema katika kipindi kifupi alichokaa ofisini, Rais Magufuli ameonyesha utendaji uliotukuka kiasi cha kuzua ari ya matumaini mapya kwa Tanzania inayoitakiwa na wananchi. Alisema tayari ameanza kuziba mianya ya upotevu mapato ya nchi na kuchukua hatua ya kupunguza matumizi ya fedha za Serikali yasiyo ya lazima.

Hadi sasa, Rais Magufuli ametekeleza baadhi ya ahadi zake alizoahidi alipokuwa akiwaomba ridhaa Watanzania ya kuongoza nchi katika kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 25.

3 comments:

Anonymous said...

JM. Baada ya wapenda haki kuanika uwazinwa ukimya wa timu nzima ya CCM. Leo unajitokeza kusema tumuunge mkono! Ukweli kabisa uko pale pale tomu yote ya kampeni na baadhi ya mawaziri waliopita hawapendezwi na kasi ya mh. Rais JPM na staili aloyokuja nayo kwani wengi walitarajia kuendelea na uzembe ule ulenwa sisi sisi wakati fedha kibao zinapotea na wananchi kukosa huduma muhimu. Kwani wote si walikuwepo kwenye awamu iliyopita na hakuna aliyegusa Majipu hayo na bado kuendelea kupokea posho.kibao na safari lukuki! Timu ya mh. JPM inabidi iwe tofauti kabisa na matarajio kwani wengi wamebobea kwenye uongozi kisa makada wa chama na mafisadi kibao ndani yake. Huu ni wakati wa kuwajali wananchi na haki iwe kwa wote. Huwezi kukaa bungeni miaka mitano posho.kibao na usiwajue wapiga kura wako hata kwa kuwapelekea maji safi. Chukueni mfano mzuri wa Mbunge wa Arumeru Nasari alibyowasaidia wapiga kura wake!! Asante JM umewadia wakati hukuwajibika basi imetosha.. Salaaam.

Anonymous said...

Watanzania wanashabikia na kusherekea kasi ya Magufuli wanaccm wanalalamika ? Na hao wanaCCM wanaolalamika ni kina nani ? Naona Makamba anataka kutupiga Kamba

Anonymous said...

Huyu makamba kuna alinitafuta sio siri na analalamika ?