Asilimia 74% ya umeme unaozalishwa China unatokana na makaa ya mawe. China ndio mtumiaji mkuu na mzalishaji mkuu wa makaa ya mawe duniani na pia ni ya pili duniani kwa utajiri na viwanda.
Tanzania tuna reserve ya tani bilioni 5 za makaa ya mawe ambayo bado hayajaguswa. Mtambo mdogo kabisa wa China unatoa MW 238 wakati ule mkubwa kabisa unatoa MW 21,310 na jumla ina vituo 25 vinavyozalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe. Mtambo wa kutoa MW 1,000 kwa mwaka unatumia wastani wa tani 1,000,000. Kwa hiyo hizo tani bilioni 5 zinaweza kutupeleka karne tano zijazo au hata tukafunga mtambo mkubwa zaidi kwa sababu makaa yapo ya kutosha. Kwa sasa Tanzania inahitaji MW 898 tu ili tusahau mgao.
Historia inaonyesha kua China ndio rafiki yetu mkubwa na wa karibu kuliko mataifa yote duniani (hawa warundi ni mizigo tu). Hivyo basi ni kwa nini tusitumie huu urafiki wetu kuwabana watujengee walau power station moja tu ya makaa ya mawe kule mchuchuma Ngaka au Kiwira?
Makaa ya mawe yanayotoka Tanzania yana madhara kidogo sana kutokana na kua na kiwango kidogo sana cha sulphur. Tukijenga kituo kimoja kikubwa cha kutoa walau MW 1,000 tu, hii itasaidia kwa kiwango kikubwa mitambo mingine iliyopo ile ya Gas powered na Hydro. Tukumbuke kua tunataka tuwe nchi ya viwanda, na kua nchi ya viwanda lazima mahitaji ya umeme yatahitajika na utatakiwa uwe wa kudumu, sio huu wa msimu kama ulanzi.
Tukishindwa kabisa basi tuwaombe ndugu zetu Waingereza watupatie Coal fired generators zao ambazo ziko nyingi hazina kazi na ikifika mwaka 2020 mitambo yote inayoendeshwa na makaa ya mawe itafungwa hapa UK. Kuliko kutupa basi watusaidie sie tujisukume nayo. Hizi Turbo Generator zao zinaishi miaka mingi kuliko binadamu, kwa hiyo tukipewa bure yanaweza kutupeleka mpaka kizazi kijacho kama yakitumiwa vizuri.
Asanteni kwa kunisoma.
NB; HAYA NI MAWAZO YANGU BINAFSI YA ;CHRIS LUKOSI

No comments:
Post a Comment