ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, December 17, 2015

PLEASE SHARE KAMA UMEKUBALI HOJA YA ZITTO


Ana mapungufu yake kama binadamu wengine, lakini huyu kijana ni moja kati ya hazina kubwa la Taifa letu na sijui kwa nini hayuko CCM.
Leo katumbua jipu kubwa sana ambalo usaha wake utaruka mpaka Monduli, NAMNUKUU;
Juzi nimewasilisha maswali 5 Bungeni ili yajibiwe na Serikali. Swali la kwanza linahusu umiliki wa IPTL na tshs 8 bilioni tunazowalipa matapeli hao kila mwezi, kwanini mtambo haujamilikishwa TANESCO na anayejiita mmiliki wa IPTL kukamatwa na kushtakiwa. Vile vile ni kwanini Benki ya Stanbic haijachukuliwa hatua kwa kuamuriwa kurudisha Fedha za akaunti ya #TegetaEscrow. Mambo 2 ( umiliki wa IPTL na kurudisha kwa fedha tshs 320 bilioni) ndio mambo ya msingi kabisa katika suala zima la #TegetaEscrow. Haya ndio nitakufa nayo.

Mwisho wa kunukuu.

Zitto ni miongoni mwa wazalendo wachache sana wenye roho ngumu ya kutoogopa. Kila mtu anajua hela zetu wenyewe, tulizoibiwa watanzania ndio zilizowapa kiburi mpaka wakaamini kua wanaweza kuchukua nchi

Ni wakati sasa Watanzania wote tuungane pamoja na kusema HAPANA

Mtu hawezi kutupiga hivi halafu tukamuacha tu aendelee kulamba asali peke yake...


3 comments:

Anonymous said...

Kwa nini aende ccm wakati yeye ni wakala wa ccm,wewe mwandishi wa makala hii vipi?aende ccm mara mbili.?

Unknown said...

Alafu eti hao wezi wa Escrow ndio wanataka nchi hapa najua unamaanisha ukawa ina maana Lowasa ndio mwizi wa Escrow? andiko hili linaonesha wewe hutumii akili

Jay said...

Sawa Escrow ni janga, ila CCM kuanzia Mwinyi mpaka huyu rubani wa ndege ndiyo wafirisi wakubwa wa nchi hii, hata mwenyewe Zitto ni mwizi wa fadhila. Anakuwa kigeugeu kwa kuchafua watu huku akilipwa na watu wake chini chini. Just imagine Zito ndiye aje kuwa rais wetu, si vituko tupu?