Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ulinzi ya Security Group Africa (SGA), Eric Sambu (kulia) akimkabidhi mshine ya kupumulia na mashuka, Mratibu wa Tiba katika Hospitali ya Mwananyamala, Dk Daniel Nkungu. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki. Katikati yao ni Meneja Mahusiano kwa wateja wa SGA, Sophia Luhikula.
Vitu vilivyotolewa msaada Hosipitalini hapo.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ulinzi ya Security Group Africa (SGA), Eric Sambu (kulia) akimkabidhi mshine ya kupumulia na mashuka, Mratibu wa Tiba katika Hospitali ya Mwananyamala, Dk Daniel Nkungu. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mahusiano kwa wateja wa SGA, Sophia Luhikula.
Baadhi ya watumishi wa kitengo cha Ambulance cha SGA
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ulinzi ya Security Group Africa (SGA), Eric Sambu akizungumza wakati wa kutoa msaada huo.
Wafanyakazi wa SGA wakibeba msaada huo.
KAMPUNI
ya Ulinzi ya Security Group (T) imetoa msaada wa mashine moja ya kupumlia na
mashuka 40 kwa wodi ya watoto katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam
Kampuni
ya SGA ilikabidhi mashine hiyo ya kupumulia na mashuka vyote vikiwa na thamani
ya Sh milioni tano kwa wodi ya watoto Hospitali ya hapo na kusema hiyo ni
kuonyesha jinsi gani wana jali afya za watanzania ambao wanafanyakazi nao.
“Nifuraha
yetu kuona familia zetu zipo katika afya njema, lakini pia ulinzi wa mali zetu
unaenda vizuri, hivyo leo tumeona tujitoe kidogo kukumbuka jamii yetu hasa
watoto ambao ndio taifa la kesho,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa SGA, Eric Sambu.
Sambu
alisema huo ni muendelezo wa kurejesha kile wanachopata kwa jamii ili kujenga
mahusiano mazuri na wataendelea kufanya hivyo kila inapo wezekana.
Akipokea
msaada huo, Mratibu wa tiba hospitalini hapo, Dk Daniel Nkungu wanaishukuru
kampuni hiyo kuwakumbuka na kuweza kuwasaidia msaada huo ambao kwa kiasi
kikubwa utasaidia ufanisi katika utendaji kazi wao na kupunguza vifo vya watoto
wachanga.
Picha ya pamoja ilipigwa
Wafanyakazi wakiwa wameshika mashuka waliyokabidhi.
Wafanyakazi wa SGA wakirejesha mashuka hayo katika boxi.
Baada ya hapo wafanyakazi walishiriki katika tafrija fupi ya kufunga mwaka na kusherehekea mwaka 31 tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo nchini ambapo awali ilijulikana kama Group 4.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ulinzi ya Security Group Africa (SGA), Eric Sambu akizungumza na wafanyakazi wakati wa tafrija.
Wafanyakazi wakimsikiliza...
Waliwasikiliza viongozi wao mbalimbali.
Wakuu mbalimbali wa vitengo walizungumza...
wafanyakazi walijumuika pamoja na kufurahi.
Chakula kizuri kiliandaliwa na watu walikula vya kutosha na kupata vinywaji vya kila namna
Watu walikula chakula na kufurahi,
3 comments:
Asanteni. ila ni kichekesho. Mashuka mengi Mashine ya oxygen ni moja. Kwa upeo wangu wa uelewa mashine hii inatumika kwa mgonjwa mmoja tu! ni bora basi mngeliacha mashuka yote na kununua walau mashine tano kama kweli lengo ni kutoa msaada kusaidia hospitali yenye mahitaji makubwa kama hii. Hebu jipimeni nguvu mongeze mashine hizi sio za gharama kubwa kiasi cha kushindwa tano! Asanteni.
Hapa naona mnajipongeza kwa kwenda mbele! maandalizi ya makabidhiano na eneo hata kama ni hospitalini imegharimu kiasi gani kwa kutoa mashine ya kupumulia moja (1)!! wahudhuriaji wa hiyo hafla ni wangapi? Duuh kweli misaada mingine waandaaji wanatakiwa kuitafakari na iwe tu kiasi cha kuikabidhi kwa ofisi ya mkurugenzi bila shgerehe, au ndio na sisi tunajulikana kutoa msaada!!
Je ni kwa jinsi gani mashuka na mashine mooja ya kupumulia kutumia oxygen inaweza kuongeza ufanisi wa kazi?? Ufanisi wa kazi ni ninyi watendaji wenyewe na sio hizo shuka wala mashine moja!!Huduma nzuri ndio ufanisi wenu!
Post a Comment