Thursday, December 10, 2015

KIFAA KIPYA CHA YANGA CHAANZA MAZOEZI DAR, PLUIJM ATAKA KUJIRIDHISHA, AMBEBA KWENDA NAYE TANGA





Mshambuliaji Issoufou Boubacar Garba 'Diego' tayari ameanza mazoezi na kikosi cha Yanga.
Diego raia wa Niger ametua nchini jana, leo ameanza mazoezi akiwa na Yanga chini ya Kocha Hans van der Pluijm.
Katika mazoezi ya Yanga yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Polisi jijini Dar es Salaam, Diego alipata nafasi ya kuonyesha vitu kadhaa.
Hata hivyo, Kocha Pluijm ameamua kumbeba mshambuliaji huyo kwenda naye Tanga ambako atapata nafasi zaidi ya kumuangalia kabla ya kupitisha uamuzi wa kumsajili au la.
Yanga inaondoka kesho kwenda Tanga ambako itakua na mechi mbili za Ligi Kuu Bara ikianza na Mgambo Shooting Jumamosi kabla ya kuivaa African Sports katika mechi inayofuata.
Mshambuliaji huyo anatumia mguu wa kushoto na anatarajiwa kuchukua nafasi aya Coutinho kama kocha huyo Mholanzi atamkubali.
Kabla ya kuja nchini, amewahi kuichezea klabu kongwe ya Tusinia ya Club African na ES Hammam-Sousse ingawa inaonyesha hakuwa akidumu katika kila klabu hata kwa msimu mmoja tu!
Source:Salehjembe

2 comments:

Anonymous said...

SAHANI,KWANZA WEKA SAWA JINA NI YUSUPH ABUBAKAR.PILI MAUMBILE NA UNENE WA SHINGO NINA WASI WASI HUYU BWANA ANATUMIA MADAWA YALIYOPIGWA MARUFUKU YA KUONGEZA NGUVU.MADAKTARI WA YANGA PIMENI MKOJO WAKE YUSUPH MTAGUNDUA. NATOA TAHADHALI KWA KLABU ZETU ZOTE TANZANIA HUSUSANI ZA LIGI KUU. MUWE MACHO NA IMPORTS MSIJE MKATULETEA TRAFFICKERS WA MADAWA YA KULEVYA.TUWE NA TAHADHARI KUBWA.DUNIA IMEHARIBIKA,

Ny Ebra said...

Kimeo mchezaji gani sasa huyu bora wangemwacha Mbrazil amalizie kuliko kupoteza pesa kwa hii shida kabisa. Mchezaji analetwa kwa mipango ya mtu minafsi maana sijaona sifa za kuvutiwa kuchezea Yanga hapa. Pole Yanga na viongozi wake wenye magengeza.