ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 16, 2015

Lowassa kuzunguka nchi nzima kuanzia kesho

Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema akiungwa
By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa ataanza ziara ya kuzunguka nchi nzima kuwashukuru Watanzania kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 na kesho atakuwa Tanga.

Katika ziara hiyo, Lowassa ataambatana na viongozi waandamizi wa Chadema na Ukawa kuwashukuru wananchi kwa namna walivyounga mkono upinzani na ajenda nzima ya mabadiliko katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene imesema kiongozi huyo atatoa shukrani zake kwa wananchi kwa jinsi wanavyoendelea kuweka matumaini yao kwa upinzani.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba wananchi bado wanaamini kwamba upinzani ndiyo nguzo imara wanayoitegemea katika kuwaletea mabadiliko ya kweli kwa ajili ya maendeleo yao na ustawi wa Taifa kwa ujumla.

“Wananchi wanastahili shukrani kwa imani hiyo kubwa ambayo ni ishara ya wazi kuwa matumaini yao kwa miaka mingine mitano yatasimamiwa na kuongozwa na upinzani imara kupitia Ukawa,” alisema Makene katika taarifa hiyo.

Alisema mbali na kupiga kura nyingi katika nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu uliopita, wananchi waliwachagua wabunge wengi wa upinzani wanaotokana na Ukawa. Alisema wabunge hao wameongeza nguvu kubwa ndani ya Bunge hususan kupitia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambayo itakuwa serikali mbadala.

Pia, alisema wananchi wameviamini vyama vya upinzani ili kusimamia na kuongoza halmashauri 34 nchi nzima, ikiwa moja ya misingi imara katika kupigania mabadiliko ambayo Watanzania wanayataka.

5 comments:

Anonymous said...

Wasting money and time. He has nothing else to do?

Anonymous said...

hiyo hela ikasaidie maji vijini,muda wa mambo hayo umekwisha sasa kazi tu!hakuna jipya unaloendakulifanya mzee wangu.

Anonymous said...

Puuuuullllliiiiiiz sir have several seats.

Anonymous said...

Huu uwenda wazimu wa Lowasa utakwisha lini? Wananchi tumekwisha msahau huyu bwana na tunaendelea na maisha yetu. Tafadhali asitupotezee muda wetu, kwani Rais Magufuli katuonyesha kweli ni Mchapakazi.

Unknown said...

At least he stop short saying that hes gonna wandering country wide declaring himself he is the president of Tanzania. Everyone knows how much this guy and his rotten mind has been addicted with the presidency so don't come be surprised on his way around the country to hear him say he is the president but on other way around Mr lowasa lookalikes at last he realized his defeat and now decide to go to the people and say good bye. We just want take this chance to advice mr lowasa and his companions on their way trip around the country is to bring Tanzanians together after the end of so called bitterly general election,instead of dividing them. Tanzania kwanza than personal interest, hope every Tanzanian is agreeing with that one. No matter where your political interest is coutry should come first.