Wednesday, December 9, 2015

Manji amwandikia barua Magufuli

“Kwa dhumuni la kutoonyesha upendeleo, katika
By Nuzulack Dausen, Mwananchi

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa kampuni ya Quality Group, Yusuf Manji amemwandikia barua Rais John Magufuli kumuelezea mchakato wa zabuni aliyoshinda kuendeleza ufukwe wa Coco maarufu kama Coco Beach uliopo Kinondoni.

Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo kwa vyombo vya habari jana ilisema Manji aliandika barua hiyo Desemba 5 mwaka huu akimuelezea kiongozi huyo wa nchi usahihi wa mchakato wa zabuni ya kuendeleza eneo hilo akiwa ameambatisha majibu ya pendekezo la mradi huo kuwa lilitakiwa kutekelezwa na kampuni tanzu ya QGL, Q Consult Ltd.

Alisema kampuni hiyo ilishinda zabuni kwa kufuata masharti na vigezo vilivyokuwa vimependekezwa na Manispaa ya Kinondoni.

Manji katika barua hiyo alionekana “kuisemelea” Manispaa hiyo kuwa Januari 20 mwaka huu QCL aliiandika barua yenye kumbukumbu namba QCL/KMC/01/15 ili kusuluhisha kesi hiyo iliyokuwa mahakamani kwa muda mrefu, lakini Manispaa waliidharau.

Alisema hakuna kipengele katika pendekezo la QCL kinachohusisha uuzaji wa ardhi wala kuzuia umma kufika kwenye ufukwe, na badala yake ilitilia mkazo mandhari nzuri kwa shughuli za kijamii na burudani kwa umma kama ilivyo katika muongozo uliotolewa na KMC na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira.

“Kwa dhumuni la kutoonyesha upendeleo, katika barua yangu kwa Mheshimiwa (Rais Dk Magufuli), niliomba afanye uchunguzi binafsi chini ya ofisi yake tukufu ambayo nitashirikiana nayo kikamilifu na nitakubaliana na hukumu ya itakayotokana na taarifa sahihi na za haki,” alisema Manji.

4 comments:

Anonymous said...

Hukumu sahihi ni kwamba coco beach ni public land

Anonymous said...

Utaisoma tu, ulishazoewa kupata kila ulichokitaka wakata wa JK

Anonymous said...

HIVI HUYU MANJI NI MWENDA WAZIMU?,KISHA AMBIWA AACHANE NA SWALA HILO LA COCO BEACH HIO NDIO SEHEMU YETU SISIWANYONGE KWENDA KUPUNGUZA GHADHIBA YA MAISHA YETU LAKINI HASIKII.

UMEOMBWA NA JAMII YOTE YATANZANIA ACHANA NASEHEMU HIO HUTAKI AU NDIO KIBURI CHA PESA? HII SASA BI SEREKALI YA MAGUFULU NA YEYE KISHA KWAMBIA ACHANA NAPO MBONA HUSIKII= KWANI WEWE NANI?

TUACHIE SEHEMU YETU

Anonymous said...

Rais ndio mwenye final say. Over.