Mhe. Balozi Masilingi alitembelea ofisi ya Bi. Cathy Byrne, Mkurugenzi Mwandamizi wa masuala ya Afrika katika Ikulu ya Marekani (White House). Wakati wa mazungmzo yao, Bi. Cathy Byrne alimueleza Mhe. Balozi Masilingi kuwa Serikali ya Marekani inaridhishwa na mahusiano mazuri yaliyopo baina yake na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Marekani. Aidha alieleza kuwa Serikali ya Marekani inaridhishwa na hatua mbalimbali zinachukuliwa na serikali ya Tanzania, katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.
Mhe. Balozi Masilingi amemhakikishia mwenyeji wake kuwa ataendeleza mashirikiano mazuri sana yaliyopo kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Marekani kwa njia ya diplomasia ya uchumi yenye lengo la kuhamasisha biashara na uwekezaji nchini Tanzania.
Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi akiagana na Bi. Cathy Byrne mara baada ya kumaliza mazungmzo yao.
No comments:
Post a Comment