Monday, December 7, 2015

MKUTANO WA MWAKA WA WATAALAMU WA MANUNUZI NA UGAVI WAFUNGULIWA JIJINI ARUSHA.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi nchini(PSPTB)Dk. Hellen Bandiho akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wataalamu unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC jijini Arusha na kusisitiza miiko ya uadilifu katika manunuzi ya umma na sekta binafsi.
Mjumbe wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi nchini(PSPTB)Ahmed Kilima akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wataalamu unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi nchini(PSPTB)Dk Clemence  Tesha  akizungumza jambo na wajumbe wa mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa taaluma ya Manunuzi na Ugavi unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC jijini Arusha na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka mikoa mbalimbali nchini na wageni kutoka nchi jirani.
Wajumbe wakiwa kwenye ukumbi wa Simba 
Wajumbe wa mkutano ambao ni wana taaluma ya Manunuzi  na Ugavi wakifatilia mada kwenye mkutano huo leo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Manunuzi  na Ugavi wakifatilia mada kwenye mkutano huo leo.
Wajumbe wa mkutano wa mwaka wa PSPTB
Mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,Dk Charles Kimei(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa fani Manunuzi na Ugavi nchini baada ya kufungua mkutano wa mwaka ambao amesisitiza umuhimu wa kufanya manunuzi sahihi yenye lengo la kuokoa fedha za umma.

1 comment:

Anonymous said...

Nyinyi Bodi ya Manunuzi ni WATU WABAYA SANA,wezi wa kupindukia na ndiye kwa makusudi mazima mnaiharibu nchi na serikali yake kwa kusababisha kwa makusudi kupanda mno kwa bei za manunuzi ya vyombo na vifaa tendea kazi vya serikali.mheshimiwa Magufuli amekwisha ligundua hili mapema na mimi naona dawa ni kuvunja bodi na kuanzisha mfumo mpya SIMPLE AND CLEAR.niwape mfano wa ubaya wenu.tenda mkiitangaza inapitia ngazi 18 narudia 18 ili mmpatie mzabuni.hiyo ni kama miezi sita.upuuzi gani huu kama si mlengo wa rushwa na kuharibu nchi.gari mpya toyota land-cruiser toka japan inauzwa [incuding c&f]kwa dollar alfu tisini,nyinyi mnampitisha mzabuni kwa dollar 160,000.wizi mtupu.hivi kweli nyinyi bodi mna huruma na nchi yenu?yaani bodi nzima ni wahujumu uchumi wakubwa na tunamuomba mheshimiwa sasa aendelee na nyiny