Monday, December 7, 2015

MWENYEKITI WA CCM JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA CCM, AKUTANA NA MWAKILISHI WA BENKI YA DUNIA

Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete akiongozana na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli , Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim. wengine ni Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Mhe samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipigiwa saluti na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015
Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015

PICHA NA IKULU

3 comments:

Anonymous said...

jee kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa,wamekutana kupokea taarifa ya mheshimiwa rais john pombe magufuli kuhusu ufujaji wa kutisha wa mali za umma,uhujumu uchumi wa kutisha na kukatisha tamaa uliokua ukifanywa na viongozi wakuu wa serikali ya awamu ya nne na jee wametoa baraka wezi wote ndani ya awamu ya nne WAFUKULIWE?hicho ndicho raia wenye shauku kubwa WANACHOSUBIRI KUONA.

Anonymous said...

I hope hawakumuita kumfunga speed gavana.

Anonymous said...

Hakuna speed governor (gavana) wala kitu kingine chochote watakachomvalisha rais na hivyo kumpunguza spidi ya utendaji kazi wake kwani Watanzania wengi wapenda amani na maendeleo ya nchi yetu tunaimani naye kubwa sana kwa vile ameonyesha dhahiri kuwa ni mkombozi wetu. Pamoja na hili pia wengi wetu, bila kujali mapenzi na itikadi zetu kichama, tunaafiki kwa kazi yake nzuri anayayoifanya kukabiliana na kero na matatizo mengine mengi na sugu ya rushwa, ubadhilifu na uzembe uliotapakaa sehemu nyingi nchini. Kwa mantiki hii sidhani kama CCM watajaribu kumhujumu wakati wanajua kuwa kwa sasa huyu ni rais wa Watanzania wote na wala siyo CCM pekee na hivyo hujuma zozote zile zinaweza zikaleta kero mpya kwa wengi tunaomfurahia na pia kuleta madhala mengine kwa chama katika chaguzi zijazo.