Advertisements

Tuesday, December 1, 2015

MWIMBAJI LADY JAYDEE KUMWAGIKA LONDON JUMAMOSI HII

Na Freddy Macha, London Mwanamuziki na mwimbaji mashuhuri wa Tanzania, Lady JayDee, anatazamiwa kutua jijini London kesho kutwa Alhamisi tayari kwa onesho kabambe Jumamosi. Akizungumza nami Jumatatu usiku, promota wa shoo hilo, Frank Leo, alisema anawaomba Watanzania na marafiki zao wajiunge kumshangilia Mtanzania mwenzetu tarehe 5 Desemba. Kiingilio cha paundi 20 ( wastani wa shilingi 45,000) kitatozwa katika holi maridadi la Oasis Banqueting Suite mtaa wa Barking, Mashariki ya London.
Frank Leo : "Shoo yake ina dhamira ya kuwaweka wana Afrika Mashariki pamoja kusheherekea na kufurahia siku ya Jamhuri, ughaibuni. Tunaiita shoo hii "Wafalme na Malkia" (Kings and Queens) maana ninaamini sisi sote ni wafalme na malkia. Lazima tukumbushane kuwa tunao uwezo kuzidi 
tunavyojua."
  
Frank Leo na bango la shughuli kadhaa za Upendo Events. Lady JayDee anatazamiwa kukaa Uingereza hadi Jumatatu tarehe 7 atakaporejea nyumbani. Mzawa wa Matombo, Morogoro, Frank Leo Mbena, anayo diploma na shahada ya usafiri na utalii kutoka hapa Uingereza alikosomea na anakoendelea kuishi. Alianzisha shirika la "Upendo Events" karibuni kujenga na kutukuza sanaa na mambo mbalimbali ya Watanzania na Waafrika Mashariki. Onesho la tarehe 5 Desemba litamhusisha pia mbunifu mavazi "All Things Africa" atakayeendesha wasanifu mavazi.  
Mfano wa mavazi yenye hulka ya Kiafrika ihsani ya “All Things African” Mkurugenzi wa "All Things African", Hamida Mbaga anachangamkia sana jitihada za "Upendo Events" na Frank leo kuitukuza na kuijenga taswira ya Tanzania nje na ndani.
Fahari ya Utanzania. Mdau wa Kitoto Blog na Meneja wa "All Things African"- Hamida Mbaga. Picha na Fab Moses Habari zaidi tembelea www.upendoevents.com

No comments: