Tuesday, December 29, 2015

NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU ATEMBELEA KITUO CHA NUNGE, KIGAMBONI

Afisa Mfawidhi Makazi ya Wazee wa kituo cha kulea watu wenye ulemavu cha Nunge Kigamboni, Bw. Ojuku Mgesi akimuonesha Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ualemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa kwanza kushoto) banda linalotumiwa kufuga kuku ikiwa ni sehemu ya mradi wa wazee wa kituo hicho.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Abdallah Possi ametembelea Kituo cha Watu wenye Ulemavu na wasiojiweza cha Nunge Kigamboni Dar es Salaam Desemba 28, 2015 ili kuangalia mazingira na changamoto wanazokumbana nazo wakazi hao.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi (mwenye miwani) akimsikiliza Bw. Salum Omari mwenye ugojwa wa ukoma alipokuwa akielezea changamoto za uvamizi wa ardhi katika Kituo cha Kulea watu wenye ulemavu na wasiojiweza cha Nunge Kigamboni. Tarehe 28, Desemba, 2015.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi akieleza jambo kwa mmoja wa wakazi wa Kituo cha Watu wenye ulemavu na wasiojiweza cha Nunge juu ya umuhimu wa kuhama na kuwapisha watu wenye matatizo wenye ulemavu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi akimsikiliza Bi. Consolata Edward alipokuwa akieleza changamoto anazokumbana nazo juu ya tatizo la Kifafa kinachomfanya wakati mwingi kupoteza fahamu na kushindwa kufanya mambo yake kwa ufasaha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments: